Elections 2010 NEC waficha taarifa za ‘voting’ na ‘counting’ kwenye mtandao wao

Mwanamayu

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2010
Posts
11,662
Reaction score
6,888
Tume ya uchaguzi imeondoa taarifa kuhusu namna ya kupiga kura na kuhesabu kura kwenye mtandao wao www.nec.go.tz .

Hii ni makusudi kuwanyima wanachi taarifa hizo kwani taarifa nyingine zipo. Taarifa hizi zitakuwa zimechakachuliwa kwenye ‘mwongozo wa kupiga kura' mfano, baada ya kupiga kura, mpiga kura anatakiwa kukaa mita 200 kutoka kwenye kituo cha kupigia kura lakini kwenye mwongozo uliosambazwa NEC inawataka wapiga kura waende nyumbani baada ya kupiga kura.

Hivi ni makusudi au ni kosa la kiufundi?
 
Hii ni hatari sana wanataka kuchakachua matokeo nadhani vyama husika wataikemea TUME haraka iwezekanavyo
 
Ushauri wangu vyama vya upinzani viibane NEC irudishe haki ya wapigakura kusimamia haki mita 200 kutoka kwenye kituo ili kuzuia mashushu ambao ndiyo wachakachuaji wakuu kuvuruga haki isitendeke.

Uchaguzi si huru wala wa haki kama hatupewi nafasi ya kujithibitishia wenyewe kama waliopo ndani ya chumba cha kuhesabia kura wanakubalika kisheria. Mashushushu siyo sehemu ya NEC ila mazingira yanajengwa ya kuiba kura.
 
Hapa ndipo pa kupigia kelele, na tusipowahi kuandika na kupiga ukunga basi watatukamata wakati tunalinda kura tukiwa mita 200. Mimi lazima nikalinde kura nitakayoipiga na mke wangu na wafanyakazi saba nyumbani kwangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…