Mhabarishaji
JF-Expert Member
- Oct 5, 2010
- 1,007
- 600
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imevishauri vyombo vya dola kutowabughudhi wananchi watakaokaa mita 100 kwenye maeneo ya vituo vya kupigia kura baada ya kumaliza kupiga kura.
Ushauri huo ylitolewa jana na Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo, Omari makungu wakati akijibu hoja iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Chadema mkoani kagera, Wilfred Lwakatare kwenye mkutano wa tume na vyama vya siasa jana.
Katika kikao hicho, Lwakatare ambaye pia ni mgombea ubunge wa jimbo la Bukoba mjini alisema kuna tabia ya vyombo vya dola ya kutumia nguvu kuwatawanya wananchi ambao hupenda kukaa kwenye vituo vya kupiga kura baada ya kupiga kura kusubiri matokeo.
Jaji Makungu alisema katika kanuni na sheria zinazoongoza Tume hakina kipengele kinachowazuia wananchi wasikae kwenye vituo vya kupigia kura.
Alisema mwananchi kukaa kwenye kituo cha kupigia kura ni hiari yake.
Makungu alisema anachotakiwa kufanya mwananchi kufanya ni kutofanya vurugu yoyote na kutokaa kwenye makundi yenye lengo la kuleta uvunjifu wa amani.
Pia alisema mgombea yeyote ana haki ya kuingia kwenye chumba cha kupigia kura kwa ajili ya kuangalia usalama wa kura zake.
CHANZO: Gazeti Mtanzania (19.10.2010)