Uchaguzi 2020 NEC yafanya uamuzi wa rufaa 616 zilizowasilishwa na wagombea Ubunge na Udiwani

Hongera NEC kwa kazi nzuri
Inawapongeza kwa kutoa ushuzi hadharani?

Kukosa sifa ya kugombea ni mambo yaliyo wazi,wala haihitaji hata wiki moja kujua kwamba, mkwepa kodi,asiye raia,aliyefunga kwa jinai hao tu ndiyo wanakosa sifa ya kugombea.

Kukosea kujaza fomu bado hakumnyimi mtu haki yake ya msingi ya kugombea uongozi
 
Kazi ya kubinya haki na kuipendelea CCM? Hata waliorejeshwa hawapewi barua za kuwaruhusu kufanya kampeni. Haki iko wapi? Karibu mwezi umepita tangu kampeni zianze, wao hawajaanza kampeni. Mnajifanya kuwa dhuluma hii hamuioni!
Sio kwamba hawana pesa mkuu!!
 
Halafu walioenguliwa ccm hamna hawajui hata kuiba
 
Nec gani inayoteuliwa na mwenyekiti mojawapo wa chama. Upuuzi mtupu
 
Ambacho sielewi kivipi mtu amegombea ubunge toka 2010 siku zote hizo fomu zipo sawa alafu 2020 ndio anakosea kujaza?

Well kakosea, huwa wanahakiki fomu je kwanini tume isikuonyeshe kosa ili uka edit au ulete kiambatanisho ila wanasubiri ukisharudisha ndio aitolee kasoro kwa kivuli cha pingamizi?

Demokrasia ni haki ya wananchi wote sio habari za kupita bila kupingwa. Walau kungekuwepo kura ya hapana na ndio sio kupitishwa tu ndio nini hiko? Tuna safari ndefu sana kufikia uhuru wa kweli
 
Kweli tumerudi nyuma kidemokrasia, 2015 waliopita bila kupingwa walikuwa 5 tu leo mwaka 2020 waliopita bila kupingwa 20 kwa trend hii mwaka 2025 si watakuwa 60?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…