Uchaguzi 2020 NEC yawateua John Shibuda na Hassan Kijogoo wa ADA-TADEA kugombea Urais wa Tanzania

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
John Shibuda anayewania nafasi ya Urais na Mgombea Mwenza Hassan Kijogoo wamerejesha fomu katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) zilizopo Jijini Dodoma.

Baada ya kujiridhisha, Tume ya Taifa imewateua wagombea hao kuwania nafasi ya Urais na Makamu wa Rais wa Tanzania baada ya kutimiza masharti.

 
Vyama vingine hivi vinajaza wingi tu
 
Unamteua Hassan Kijogoo halafu usimteue Lissu ......... hayo ni maajabu ya Dunia!!
 
Hawa tissue papers hata muda wa kuwafuatilia hatuna.
 
Hawa wapo kwenye uchaguzi kwa sababu maalum.
Iwapo Lisu akikataa kutambua matokeo yamwisho yatakayotangazwa na tume, hawa kina Kijogoo watayakubali na watakuwepo siku ya kuapishwa Rais mteule wa Tume.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…