KIDUNDULIMA
JF-Expert Member
- Aug 18, 2010
- 966
- 540
Vijana ninaowazungumzia ni wale ambao TCU imewatangaza kuwa hawana sifa za kuchaguliwa kujiunga vyuo vikuu kwa vile hawa sifa kwa vile hawana credit tatu za O-level. Vijana hawa wengi wao ni wale waliosoma kwa taabu sana katika shule za Kata na wengine wakapata CIV-D; HIST-D; GEO-D; KISW-B; ENGL-C; PHY-F; CHEM-F; BIO-F; B/MATH-F: mwingine amepata CIV-D; HIST-C; GEO-D; E/D/KIISLAMU-F; KISW-D; ENGL-D; BIO-D; B/MATH-; na mwingine kapata CIV-D; HIST-D; GEO-F; KISW-C; ENGL-C; PHY-F; CHEM-D; BIO-F; B/MATH-D na wengine wengi amabao siwezi kuwataja. Vijana hawa waliruhusuwa na NECTA kufanya mitihani na kidato cha sita kwa sababu wengi wao walikuwa wamechaguliwa kujiunga na shule za serikali maana wangeenda shule za private wasingekubaliwa kufanya mitihani kwa vile hawana credit tatu. Kuna vijana ambao TCU wamewataja kuwa hawa wana sifa za kuomba na kuchaguliwa, baadhi yao kwa vile tu wana credit tatu za o-level baadhi matokeo yao ya O=level ni kama CIV-C; HIST-D; GEO-C; KISW-C; ENGL-F; BIO-F; B/MATH-F; na mwingine CIV-D; HIST-F; GEO-C; KISW-C; ENGL-C; BIO-F; B/MATH-F. Haya makundi ukifuatilia sana walio na credit tatu na wasiokuwa nazo ni kama sifia zao zinalingana na mara nyingine wasiokua na credit tatu kuwa na point nyingi zaidi katika ujumla wa masomo waliyofaulu (A=5, B=4, C=3, D=2, F=0). Sasa kama baraza waliwaruhusu vijana kufanya mitihani sijui kwa kigezo kipi kwa nini TCU wasiwaruhusu wajiunge na vyuo kama sifa za A level zinawaruhusu?