NECTA Yabadilisha Viwango vya Ufaulu Form 6, DIV I Mwisho point 7

Jerindeo

Member
Joined
Aug 15, 2013
Posts
74
Reaction score
33
NECTA imetoa mwongozo wa matumizi ya viwango vya Ufaulu (Aprili 2014) ambao umesambwazwa katika shule zote ze sekondari kupitia kwa Maafisa Elimu wa Mikoa. Kwa mujibu wa mwongozo huo Madaraja ya ufaulu kwa Kidato cha Sita 2014 yatapangwa kwa kutumia mfumo uliooneshwa kwenye ukurasa wa 8 wa mwongozo huo ambao ni:
Div I pointi 3-7
Div II pointi 8-9
Div III Pointi 10-13
Div IV awe na D mbili au C moja
Div 0 aliyepata chini ya D mbili.

Kwa mujibu wa mwongozo huo masomo yatakayohesabika kwenye kupanga pointi ni yale tu yaliyoko kwenye tahasusi yaani combination. Kwa maneno mengine suala la kupata cheti kwa mgongo wa Bible Knowledge au Islamic Knowledge litakuwa halipo tena.

Kuanzia Kidato cha Nne 2014 na Kidato cha Tano Sita 2015 mfumo wa GPA utatumia. Kwa maelezo Zaidi soma kurasa wa 8 na 9 na pia unaweza kukipata kijitabu hicho toka shule yoyote ya sekondari au kwenye ofisi za elimu za mkoa na wilaya.
 

Attachments

Wenzangu na mie waliokuwa wanategemea masomo ya dini sasa watakiona. Go NECTA gooooooo!!!
 

Itatusaidia kuinua ubora wa elimu yetu
 
div one wameibana xana

Div II vipi, pointi 8-9 hapo ndiyo wameachia eeeh! Ila mkizoea vya kunyonga na vya kuchinja mviweze. Mlipokuwa mnafurahia thamani ya alama za grade kushushwa mlitegemea nini?

Angalau Bodi ya Mikopo itapumua maana watakaoweza kupata mikopo watapungua
 
Mwaka huu kuna vyuo vikuu vitakosa watu!
 
Duuuh hivi hawa Necta uuuuwi mbona wanatupa pressure aisee div 1 wameifinya mh na two...daaah haya ni majanga negative
 
Maajabu hayatakaa yaishe nchi hii. Yaani NECTA wanatoa mwongozo baada ya wanafunzi wa Kidato cha sita 2014 kumaliza mitihani yao?

Halafu eti mwaka 2015 mfumo utakuwa tofauti watatumia GPA. Ni vema watuambie 2016 watatumia mfumo upi na kwa nini wawe wanabadilisha kila mwaka kwani hii mifumo mingine ina matatizo gani?
 
Wenzangu na mie waliokuwa wanategemea masomo ya dini sasa watakiona. Go NECTA gooooooo!!!

Mimi napenda sana hawa wanaotegemea masomo ya dini Inshaalah mwenyezimungu awape moyo huo huo wewe endelea kuipenda hii dunia yenye kuisha.
 
Duh. Div 111 point 10-13??
Mbona ni janga hilo maana hizo point zimebanwa. Khaa!
 
Wenyewe walifauru kwa mifumo ya zamani....sasa sisi ndio wanatunyonga....mala mikopo kwa arts cutoffs 4.0....yan n majangaaa matupu TZ
 
Hawa jamaa si fair kabisa yani D mbili ni dv4 na chini ya D mbili ni dv0
 
Hakuna cha vyuo kukosa watu kwani hata grade zimebadilika wakuu so utakuta d ya last ti e ni B ya sasa na B+ ya sasa ni c ya zamam so changes nii kama hakuna
 
Angalau watu wataacha kilele mtaani maana zilikuwa zimezidi kiasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…