Necta yaikana serikali mtihani darasa la Saba

Necta yaikana serikali mtihani darasa la Saba

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
James%20mbatia.jpg

Mbunge wa Kuteuliwa (NCCR-Mageuzi), James Mbatia.

Wakati Wizara ya Elimu ikikwepa juu ya kuboronga kwa mitihani ya majaribio ulioibuliwa na mbunge wa Kuteuliwa (NCCR-Mageuzi), James Mbatia, NIPASHE imebaini kwamba madai kuwa waliotunga mtihani huo ni Baraza la Taifa la Mitihani (Necta),siyo ya kweli.
Jana, Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi, alikaririwa na gazeti moja(siyo NIPASHE), akieleza kuwa mitihani ya majaribio iliyofanyika mwezi uliopita ulitungwa na Necta na kwamba mtihani aliuounyesha Mbatia ni feki kwa kuwa sio ambao wanafunzi waliufanya.
Hata hivyo, jana Necta limekana kutunga mtihani huo na kueleza kwamba hutunga mitihani minnepekee.
Msemaji wa Necta, John Nchimbi, aliiambia NIPASHE jana kwamba baraza hilo halihusiki kutunga mitihani yoyote ya majaribio kwawanafunzi wa ngazi zote.
“Necta inatunga mitihani minne tu ambayo ni wa kumaliza darasala Saba, kidato cha Nne, kidato cha Sita na Ualimu,” alisema.
Mapema mwezi huu, Mbatia aliibua madudu kwenye mtihani wa majaribio wa darasa la saba, uliofanyika Julai, mwaka huu katika wilaya 40 za Tanzania Bara kuwa na mapungufu makubwa na ya wazi.
Aidha, maswali 12 kati ya 50 katika mtihani wa Hisabati hayana majibu, 14 ni magumu ambayo mtoto wa darasa la sabahawezi kujibu na mengine matano yamekosewa na hata yafanywe kwa kiasi gani hayawezi kuwa na majibu.
Mbatia aliwaomba Watanzania kushiriki kupinga anguko la elimu linalotia aibu Taifa.
Mtihani huo ulifanywa Julai 08 na 09, mwaka huu, kwa masomo ya Hisabati, Kiswahili na Kiingereza na kwamba baada ya kupata mtihani huo, alikusanya baadhi ya walimu wa shule za msingi na sekondari katika moja ya shule jijini Dar es Salaam na kufanya mtihani huo zaidi ya nusu walishindwa kupata daraja la tatu yaani C.
CHANZO: NIPASHE
 
Elimu yetu kwa ivi sasa inamatatizo makubwa, hata kama hawa husiki na huo mtihani. Issue ya msingi wana mipango ipi ya kuhakikisha kiwango cha elimu hakishuki kama miaka ya hivi karibuni..
 
Back
Top Bottom