NECTA Yatangaza matokeo ya darasa la Saba. Shule 38 zafutiwa matokeo kwa udanganyifu

PAZIA 3

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
1,102
Reaction score
1,919
MATOKEO YA DARASA LA 7 YATANGAZWA. SHULE 38 ZAFUTIWA MATOKEO KWA UDANGANYIFU

Baraza la Mitihani nchini #Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kuhitimu Elimu ya Msingi ambapo limezifutia matokeo Shule 38 za Msingi kutokana na udanganyifu uliofanyika wakati wa Mitihani hiyo ya Taifa

Shule hizo 38 kati ya 17,329 ambazo zilifanya mtihani, ziligundulika kukiuka Kanuni na Usimamizi wa Mitihani baada ya Wanafunzi 1,059 kuonekana kuwa na ufanano mkubwa wa majibu. Shule hizo ni kutokea Mikoa ya Geita, Morogoro, Simiyu, Arusha na Tabora

Soma pia matokeo mengine kuanzia mwaka 2008
===
Kupitia Facebook page ya NECTA, katibu mkuu ametangaza matokeo ya darasa la Saba, ingia kwenye website ya NECTA

RESULTS


 
Hivi ni mwisho grade gani mtoto anaweza kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza?
 
Mfano wa majibu sahihi na mfanano wa majibu kwa njia za udanganyifu viko wazi kabisa...
 
Kama wote wanajua majibu kwa uhakika sasa kwanini wasipatie..?
Hapo sioni mantiki
 
Hapana aseee kwa hiyo Kama Jibu linajulikana Ni A na wanafunzi wote wanajua hivyo Sasa hapo Kuna ubaya gan wawaache watoto waendelee mbele bana

Sent using Jamii Forums mobile app
Kufanana ktk kupatia huwaga hakuna shida ila kufanana ktk kukosea ndio kunaibuaga kufutiwa matokeo haiwezekani jibu liwe A halafu wanafunzi 60 wote wa shule moja waandike B na wakati Kuna machaguo manne wakifanana ktk kukosea maswali zaidi ya matatu hapo kuna tatizo kunaashiria udanganyifu umetokea
 
Mtoto wa mchepuko wangu kapiga B ya Maarifa ya Jamii na masomo mengine yote A. Nawaza zawadi ya kumpa lakini inategemeana na baba yake atampa zawadi gani kwanza
 
Wakapige msuli walio bahatika
Ila big up ziende kwa walio feli wakalekebishe michongo kitaa ili wawe mwanga wa wanao soma
 
Mtoto wa mchepuko wangu kapiga B ya Maarifa ya Jamii na masomo mengine yote A. Nawaza zawadi ya kumpa lakini inategemeana na baba yake atampa zawadi gani kwanza

[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Mbona awamu hii shule kutoka lake zone zinaongoza sana?
 
Hongera kwa watoto wetu, wazazi, walezi na serikali kwa matokeo mazuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…