Need for speed ii, karibu tushindane online kwa internet tujikumbushe enzi za 2000s

Need for speed ii, karibu tushindane online kwa internet tujikumbushe enzi za 2000s

Start-Menu

Member
Joined
Sep 10, 2023
Posts
14
Reaction score
66
Mods tafadhalini msiunge na nyuzi zingine, hili ni toleo la online version

1720276086850.png


Hapo zamani tulizoea kucheza wawili kwa screen kugawanywa lakini kwa mapinduzi ya teknolojia tunaweza kushindana online kwa kutumia internet na MB chache sana.

KUDOWNLOAD NA KUCHEZA GAME

Game _MB 128 tu) >>> Download Hapa ,<<<<

Kucheza game fungua nfs2se.exe



Endapo ikileta shida au kukwama minya file la "config.exe", Nenda sehemu ya renderer, settings zilizokuwepo ni Direct X 8, jaribu kushusha direct x kama 7, 6 na 5 kisha minya save jaribu kufungua tena game.




Kama pc yak ina uwezo zaidi unweza kujaribu Nglide, Open GL1 na Open GL 2

Game inapokwama na screen kuwa nyeusi mfano settings zilizopo zinagoma ama unapobadili settings, kwenye keyboard minya Ctrl, Alt na Delete kwa mpigo, Minya Sign out kisha anza kuminya mara nyingi esc, kisha badili settings za renderer.

KUSHINDANA MBIO ONLINE

1. KUSETI KWA MARA YA KWANZA


Install Program ya Radmin, Imo kwenye folder la Radmin


Hakikisha upo online na kuwe na alama ya on.



Sehemu ya Network Minya "Join Network"



Ingiza Username na Password za network

Mfano Network ya mashindano kwa watanzania niliyotengeneza

Username: Nfs2tz
Password : pamoja


Fungua Game nenda "game setup", sehemu ya "game type" chagua "network" minya "done"

minya "CONNECT"

minya "Create Game"

Baada ya hapo funga game, utaona kuna ujumbe huu minya allow access



Kuanzia hapo utaweza kushirikia mashindano onlline

2. KUJIUNGA MASHINDANO YANAYOANDALIWA NA WENGINE

Anaeandaa shindano inabidi wote muwe kwenye networlk moja mfaano "nfs2tz"

awape ip adress yake ya Radmin, Mfano mimi nikitaka kuandaa shindano nawapa yangu 26.31.167.174


Fungua Game nenda "game setup", sehemu ya "game type" chagua "network" minya "done"

minya "CONNECT"

minya "Join Game"

Ingiza ip adress uliyopewa na alieandaa shindano mfano 26.31.167.174

Hapo utaweza kuwaona wengine waliojiunga na kushindana

3. KUANDAA SHINDANO

Unaotaka kuwaalika mshindane hakikisha wote mmejiunga network husika, mfano Nfs2tz

Wape Ip adress yako unayoiona kwenye Radmin vpn

Fungua Game nenda "game setup", sehemu ya "game type" chagua "network" minya "done"

minya "CONNECT"

minya "Create Game"

Hapo utaweza kuwaona wengine waliojiunga na kushindana
 
Nzuri hii, ukiweza kuconfig ya NFS Underground 2 itakua poa sana mkuu.
 
Back
Top Bottom