Neema yawashukia wakulima

Neema yawashukia wakulima

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
3,925
Reaction score
8,853
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema serikali inatambua umuhimu wa wakulima nchini katika kuisaidia nchi kuwa na chakula cha kutosha.
Rais Samia ameeleza hayo Jijini Dodoma wakati wa Kilele cha Maonesho ya NaneNane.

Amesema ndio maana serikali imeamua kujenga Viwanda ikiwamo cha kuunganisha Matrekta yatakayosaidia kufanya kilimo kwa urahisi.
Amewataka wakulima na wafugaji kuishi kwa amani na kupunguza migogoro isiyo na ulazima.
Sambamba na hayo amewataka maafisa ugani kuitumia vizuri taaluma yao katika kuwasaidia wakulima kufanya kilimo chenye tija.

Akihitimisha hotuba yake amewataka wananchi kuchagua viongozi madhubuti watakaowasaidia wananchi kupata maendeleo.

Maadhimishi ya Nanenane yamehudhuriwa na Viongozi mbalimbali pamoja na wadau wa maendeleo nchini.
 
Ni nilijua ametoa pesa ili kijengwe kiwanda cha Mbolea Nyanda za juu kidini😲
 
Back
Top Bottom