Neman chilomo alipotelea wapi?

Neman chilomo alipotelea wapi?

ebaeban

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2012
Posts
2,205
Reaction score
2,697
Kama ndio kitu mission kuwa perfecf basi mission aliyofanyiwa jamaa huyu ilikuwa babu kubwa,

Neman Chilomo
alisoma Bihawana sec.school miaka ya 70 na baadae Mzumbe A LEVEL. Alikuwa mwenyeji wa Dodoma (mgogo) wa kijiji cha Kigwe-Dodoma vijijini sasa hivi ni wilaya ya BAHI.Baada ya kumaliza shule enzi hizo miaka ya 73 aliajiliwa shirika la reli wakati huo ni jumuia ya africa mashariki, kituo chake cha kwanza cha kazi ilikuwa pale Dar-es-sallam alikuwa akiishi quater za railway eneo la gerezani.

Mwaka 1975 mwezi fulani sikumbuki ila saa za jioni inasemekana aliondoka nyumbani kwake ili kwenda kwa jirani yake ambaye alimwazima kitabu cha hesabu na walikuwa wanafanya nae kazi, kwa bahati mbaya alisahau kitabu cha bank humo kitabuni (zile pass book za zamani ) sasa nia ya kwenda kwa jirani yake huyo ambapo siyo mbali na alipokuwa anakaa Neman ni kwenda kuchua hiyo pass book yake ili akachukue hela bank kesho yake. NEMAN CHILOMO kwa rafiki yake hakufika wala nyumbani kwake hakurudi mpaka leo hii tarehe 28/2/2013 yapata miaka 38.

Alikuwa mtoto wa pekee kwa mama yake Mama Neman alikuwa anaishi kijiji cha Kigwe Dodoma. Mama huyo alilia akanyamaza , alimtafuta weee,hakupatikana story na story kuhusu Nerman zilisimuliwa. Neman hakuonekana alipotea kabisa sijui yuko hai sijui amakufa haijulikani . kwa umri sasa angekuwa na miaka 63.
Mama yake amakufa kama miaka 5 imepita

Mwenye tetesi kuhusu huyu jamaa habu alete mchango wake hasa wafanya kazi wa railway wa afrika mashariki. Wabaya wake kwa nini walimfanyizia walikuwa na kisa gani na yeye? wanye tetesi tunaomba.
 
Kweli inasikitisha sana. Kwa miaka hiyo population ya DSM ilikuwa ndogo sana na crime level ilikuwa ni ndogo pia!!! Je alikuwa anajishughulisha na Siasa za wakati ule? Watumishi wengi wa serikali walikuwa ni nyoka vile vile (lugha ya fasihi). Hakufanya kosa lolote kwa chatu? Maana kama ukimkosea chatu ni lazima utoweke!!!
 
Kweli inasikitisha sana. Kwa miaka hiyo population ya DSM ilikuwa ndogo sana na crime level ilikuwa ni ndogo pia!!! Je alikuwa anajishughulisha na Siasa za wakati ule? Watumishi wengi wa serikali walikuwa ni nyoka vile vile (lugha ya fasihi). Hakufanya kosa lolote kwa chatu? Maana kama ukimkosea chatu ni lazima utoweke!!!

Mi nadhani alichukuliwa msukule kwa kumbukumbu zangu hilo jina halikuwahi kugusa siasa labda kama kulikuwa na cold war ndiyo tunaweza sema system ilifanya vitu vyake.
 
Back
Top Bottom