NEMC fanyeni kama Polisi au Jeshi la Uhamiaji

NEMC fanyeni kama Polisi au Jeshi la Uhamiaji

Faana

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
38,657
Reaction score
44,759
Mitaani kumechafuka hivi sasa
  1. Vigodoro vinakesha kwenye makazi ya watu serikali za mitaa zimetiwa mifukoni mwa watu
  2. Makanisa yanafunga speaker kubwakubwa zisizotofautiana na zile za kumbi za disco kwenye open space
  3. Bar nazo zinasumbua usiku kucha miziki mizitomizito kwenye makazi ya watu
  4. Wauza CD, vinyozi, wauzaji wa vyombo vya muziki nk nao wameshika kasi
Tuweke vipaumbele katika kulinda afywa za wakazi na kuzuia kelele chafuzi na mitetemo kwenye makazi ya watu.

Hakuna ulazima wa vigodoro kufanyika kwenye makazi ya watu wakati sherehe zinaweza kufanyika kwenye kumbi za starehe.

Hakuna ulazima wa mitambo hiyo kufungwa kwenye makazi ya watu halafu sauti inakwenda umbeali wa mita 500+

Nawashauri NEMC fanyeni kama Polisi na Uhamiaji, wakisikia sehemu kuna gongo, magendo au bangi na wahamiaji haramu hawasubiri barua ya malalamiko kutoka kwa wakazi wa eneo husika, nanyi nemc mkisikia kelele chafuzi nendeni mkawadake wahusika ili kupunguza kero mtaani.

Kipindi hiki wanafunzi wengi wapi likizo wanahitaji muda mwingi wa kujisomea, lakini uuzwaji holela wa vyombo vya muziki umekuwa kero kubwa kwa wakazi walio wengi mijini na vijijini.

Tunaomba NEMC tumieni ujuzi, ubunifu, uadilifu, uzalendo nk kukomesha adha hizi zinaota mizizi.
 
Back
Top Bottom