hsnaturalfertility
JF-Expert Member
- May 14, 2022
- 399
- 992
Wananchi wa Ilemela Mwanza tuna taabu kubwa, hapa naandika hii thread ni saa sita usiku, hawa Kwa Tunza lodge wanapiga muziki sauti ya juu sana hakuna kulala. Tena leo wamemualika DJ AllyB kila saa "Nasemaje", yaani tunasubiri alfajiri wakimaliza labda ndio tutalala.
Huyu Salum mmiliki wa Kwa Tunza anatoa wapi jeuri ya kudharau maagizo ya NEMC? Yeye ni nani? Yuko juu ya sheria? Naomba NEMC mtembelee hapo mahali maana hata lodge yake kaijenga ziwani kabisa, hakuna usalama kwa wateja. Ila anzeni na hilo la sauti kwanza.
Ikishindikana NEMC kulifanyia hili kazi tutaenda mamlaka za juu kabisa, haiwezekani tuteseke kwenye nyumba zetu tulizozijenga kwa taabu sana.