Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 38,657
- 44,759
Kiukweli hali imekuwa mbaya sana mtaani, vyombo vya entertainment majumbani na sehemu za starehe vinazidi kuongezeka kwa kasi na sasa imefikia familia na wenye bar pamoja na makanisa wananunua maspika makubwa yanayotakiwa kufungwa kwenye kumbi za muziki yanawekwa majumbani na kwenye sehemu za starehe bila kuzingatia kuwa ni makazi ya watu na kuzisababishia familia nyingi usumbufu.
Napendekeza kama ikiwapendeza NEMC, maafisa wenu walioko kwenye miji wanunuliwe sound meters ambazo watafanya nazo doria kimyakimya na kusoma miziki inayozidi viwango na kuwatoza fine wahusika.
Hii itasaidia kukomesha tabia ya watu kupiga miziki na kuchafua mazingira kadhalika itaongeza mapato kwa serikali kama wanavyofanya askari wa usalama barabarani wanapowakamata madereva wazembe.