Hii mchi imekuwa nchi ya hovyo sana. Kila mahali ni makelele tu.
Makanisani
Maana ya kuwa na kanisa ni kuwa na eneo maalumu la kukusanyika na kusali au kuomba na kuambiana yanayowahusu waliopo pale. Lakini utakuta wamefunga maspika yenye nguvu kusambaza sauti hadi umbali wa kilomita 2 hadi 3. Haijalishi ni usiku au mchana. Hii imekuwa ni kero kwa nchi nzima NEMC mnatakiwa muwajibike katikakukomesha hii tabia. Mwenye shida ya kusikia hayo mahubiri atasogea hapo kanisani kusikililiza sio kuwalazimisha watu kusikia wasichotaka kusikia. Mbona makanisa mfano wasabato SDA, warumi RC, waluteri KKKT/ELCT hawana mambi hayo ya maspika yenye makelele makanisani na wanamwabudu Mungu?
Misikitini
Hawa nao wamekuwa kero asubuhi, sijui nani aliwaambia wakati wa ibada zao wote tunahitaji kuamshwa. Waweke alarm muda wa kuamka tusisumbuane kwakweli. NEMC mnanisikia.
Japo hawa wakati wa ibada zao hawasumbui sana na masipika. Lakini cha kujiuliza mbona Jamatini hakunaga makelele na wanaabudu?
Sokoni na minadani
Hii kero sasa ndio usiseme, limekuwa ni janga la kitaifa. Yaani masokoni kila sehemu unayopita ni makelele ya vipaza sauti mpaka hauwezi kusikia hata kinachotangazwa. Ni sauti tu zinaingiliana hazina maana yoyote. Nataka haraka sana NEMC wapige marufuku hili jambo likome. Mfano Kariakoo soko la kimataifa, Karume na maeneo mengine nchini huu upuuzi umeenea. NEMC muwajibike haraka.
Studio za miziki na video/movies mtaani
Janga lingine hilo. Usiombe ukawa karibu na hawa jamaa na maspika yao. Ni kero na sijui kwanini hata serikali za mitaa wanafumbia macho hili jambo. Ni kero ya makelele mtindo mmoja. NEMC saidieni kuondoa hili. Msisubiri hisani ya watu wa Marekani USAID.
Vyombo vya usafiri, magari na pikipiki.
Unakuta wamefungulia sauti juu ya muziki au movie mpaka vichwa vinauma. Hauwezi kupiga simu au kufanya maongezi na mtu ndani ya chombo cha usafiri.
Pia utakuta kidhibiti sauti cha bomba la kutolea moshi wa gari au pikipiki kimekufa au mtu kakiharibu makusudi ili apige kelele mtaani watu wamwone. Sheria zipo kudhibiti haya yote, NEMC komesheni huu upuuzi.
Kumbi za starehe na harusi
Hili ni janga maeneo mengi ya nchi hasa mabaa ya kawaida na ya kukesha. Pia kumbi za harusi. Hawa watu wanatakiwa kuweka vidhibiti sauti lakini hili mnaliacha tu na kuangalia wananchi wakisumbuliwa. Nataka kuona NEMC mkichukua hatua.
Mwisho
Nawaagiza NEMC msimamie sheria zilizopo kuondoa hizi kero. Wahusika wafuate sheria kudhibiti sauti za maeneo yao zibaki kwa wanufaika au wafungiwe na kupigwa adhabu wasipotekeleza matakwa ya sheria. Na kufunguliwa kwao ni mpaka wakidhi vigezo.
NEMC timizeni wajibu wenu, mkiwajibika hizi sio kero, zinasababishwa na uzembe wenu tu.