Bila ya kukwaza kwa makusudi.....naona niungane nawe kwa mtazamo wako.
Inaweza kuwa kweli kama Bodaboda hizo hukaa eneo moja kama baa zilivyo na kupiga makelele za muziki .
Ukweli...
Bodaboda huwa zinapita, na kufanya makelele hayo kuwa ni ya muda mfupi tu ukilinganisha na Baa zilizo sehemu ya makazi ya watu ambazo ni wakati wote baa huwa zimefunguliwa.
Ukweli....
Ikiwa makazi yapo karibu na barabara au Bodaboda zinafikia maeneo ya makazi na makelele hayo.
Hatahivyo....
Suala la watu kujenga makazi karibu na barabara yakikoma- na ikiwa kuwa hilo haliwezekani kutokana na sababu zisizoweza kuzuilika, basi wajenge kuta za kudeflect mirindimo ya magari, pikipiki (bodaboda), n.k Vilevile ikiwa Pikipiki zenye miziki zikifika maeneo ya makazi basi wahakikishe wanazima au kupunguza sauti za miziki yao.
Kama ni kweli ni sauti ya muziki wa Bodaboda na wakati huo huo Bodaboda imetumika hapa kama ikimaanisha pikipiki, basi Pikipiki zote zenye sauti ya muziki munene zikomeshwe...ila kama inamaanisha Bodaboda kana Wafanyabiashara wanaotumia pikipiki, basi kuna uwalakini kuhusu kutumia suala la makelele ya Baa kuuzima na kudumuza Biashara-i.e ya Bodaboda.
Kwa namna moja au nyingine utaona hapa ndipo muingiliano wa hoja za kuwa na 'uhuru na haki ya kuongea' dhidi ya 'haki ya kuwa na faraga' na yale ya 'Umasikini wa kufukuza upepo' Kwa mtazamo wangu
Suala la Muziki au makelele ya Baa yasitumike sambamba na masuala ya kutaka kuzima biashara za wanaojiajiri ili kuwapa watu wenye mitaji mikubwa kukwapua soko la usafirishaji watu mjini.
yaani A monopoly.
Kwa namna moja au nyingine watumie masuluhisho bila ya kuwa na athari na madhara hasi kwa Wafanyabiashara walio na mitaji midogo. Tusipeane Umasikini kwa madai ya Kufukuza Umasikini
🙄