baraza la usimamizi wa mazingira NEMC mimi binafsi nashindwa kuwaelewa.
Juzi Juzi walipiga marufuku machinga eneo la jangwani lakini eneo hilohilo kumejengwa karakana nasikia ya BRT sijasikia wakiisema.
Juzi kwenye vyombo vya habari nimesikia wakifunga kiwanda cha Kusindika nyama ya punda kwa na kwa hoja hii ya kiwanda cha kusindika nyama ya punda mimi niliishangaa serikali
1. wawekezaji wa namna hii kwa maana viwanda vinavyojengwa vikilenga kupeleka bidhaa zake 100% nje ndio first priority kwetu.
2. wanyama wanaosindika sisi kwetu hatuli, wamekuwa wakitumika kubeba mizigo basi sasa tumepata soko la bidhaa tuliharasi.
3. nemc kwanini wasiwatembelee wawekezaji kama hawa wakawaelimisha kwanza na kuwaelekeza jambo la kufanya na sio mmelala mkikurupuka mnatisha watu, mnawaharasi kwa vyombo vya habari mkiwachafua na kuwaharasi na vyombo vya usalama. jambo la kijiuliza hapa ni wao walikuwa wapi mpaka kiwanda kinajengwa na kinafanya kazi bila kujali mazingira na siku moja wanaibuka na nguvu zote hizo.
kama walivyokuwa wamesinzia nemc ndivyo wawekezaji wanavyoweza kusinzia hivyo si swala la wewe kukurupuka usingizini na ukamharasi mwenzako ambaye mlikuwa mmesinzia wote.
hapa ninachojaribu kusema ni ili tupige hatua za kimaendeleo ni lazima taasisi zetu zote zitambue wajibu wao kuwa kila taasisi inawajibu katika kujenga uchumi wetu. mnaweza kuweka mipango mizuri ya kuvuta wawekezaji lakini huku taasisi nyingine ya kwenu inafanya kazi ya kufukuza wawekezaji ikijifanya iko bize na majukumu yake.
hebu tuangalie wananchi mbeya, tarime na maeneo mengine wamelalamika mara ngapi juu ya migodi kuchafua mazingira kiasi cha binadamu kuathirika, hivi wamechukua hatua gani kwa migodi ya giant investors. sasa nalinganisha jinsi damu inayotiririka, kuchoma mifupa vinavyohatarisha mazingira kiasi cha kuona yale tuliyoyaona.
sisemi nemc wasifanye kazi yao lakini mfumo wao wa kufanya kazi mimi naona ni kama wachezaji walioko uwanjani bila kujua goli lao ni lipi hivyo wanabutua mipira kuelekea popote na uwezekano wa kujifunga ni mkubwa.
haya yote yanatokea kwa sababu shughuli za serikali zinakosa coordination na kuunda taasisi ya kupanga na kusimamia uchumi ili iwe inatoa mwongozo kwa kila taasisi ya serikali ili wote watimize wajibu wao kwa kushirikiana na sio kugongana.