KERO NEMC na Serikali za Mtaa, Wilaya ya Ilemela mmeshindwa kudhibiti kelele?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mkazi wa Nyasaka, kata ya kawekamo, wilaya ya Ilemela, Mkoa wa Mwanza.

Kero yangu kubwa ni wimbi la kelele zilizopitiliza kwenye makazi ya watu zinatoka kwenye nyumba za ibada, sehemu za starehe na wafanya promotion za biashara na makazi ya watu wanapofanya sherehe za harusi.

Imekuwa ni kawaida sasa kwa maeneo mbalimbali ya wilaya za Nyamagana na Ilemela (Mwanza) kukuta kuna uchafuzi mkubwa wa kelele katika makazi ya watu.

Jambo hili limekuwa sugu licha ya kwamba kuna sheria zimetungwa kudhibiti kelele na mitetemo na pia kuna mamlaka zimepewa jukumu hilo la kufatilia na kudhibiti kelele ila ni kama wamelala na hawajishugulishi nalo kabisa, wananchi ndio tumekuwa wahanga wa kelele hizi.

Serikali za Mtaa kuanzia mwenyekiti wa mtaa ambaye ndio mtu wa kwanza kudhibiti kelele wamekuwa hawajishughulishi na jambo hilo, ofisi za kata, Idara ya mazingira, Halmashauri ya Ilemela na Baraza la taifa la mazingira (NEMC) nao wamekaa tu maofisini huku mtaani wananchi tukikosa utulivu tokana na kelele zilizopitiliza kwenye makazi ya watu.

Mfano eneo nalokaa mie la Nyasaka msumbiji kuna kanisa la walokoke linaitwa Bethel linapiga muziki karibia kila siku kuanzia Jumatatu mpk Jumapili. Jumamosi wanapiga muziki kuanzia saa tatu asubui mpk saa tatu usiku hata kama hakuna watu kanisani, wanachofanya ni kuunganisha simu kwenye spika kisha wanafungulia sauti kubwa.

Wauza vilevi/pombe nao wakiamua weekend nzima kuanzia saa moja ni mziki mnene, hapo bado hawajaja watu wa promotion kutangaza bidhaa zao.

Pia mtu ana sherehe kwake anafunga mziki mnene usiku mzima hata siku mbili bila kujali watoto,wagonjwa,wazee na majirani wanaohitaji utulivu ili wapumzike.

Kero hii ya kelele imefanya tuchelewe kurudi majumbani kwetu ilimradi tukute washazima mziki. Siku za kupumzika nyumbani ni kero tupu zitokanazo na kelele.

Natoa wito kwa serikali na taasisi zake waliopewa dhima ya kuzuia uchafuzi huu wa kelele watimize majukumu yao,kwan kelele hizi zina athari kubwa kiafya na kijamii pia. NEMC NA OR TAMISEMI ni muda sasa wakachukua hatua na kusimamia sheria dhidi ya kelele hizi.
 
Hakikaa n kero, SEMA ndio wafatiliaji n wapo busy na kupokea rusha Ili kelele ziendeleee.
 
Kama hutaki kelele hama mjini, nenda kaishi huko porini Serengeti. Maisha ni kuvumiliana watu hawawezi kuishi kama unavotaka wewe iwe. Kumbuka na wewe Kuna watu unawakera sema ndo ivo wanakuvumilia.
 
Kuna ule mtaa wanauita Ghana, karibia na Rock City Mall, aisee kelele za muziki kuanzia Ijumaa mpaka Jumapili sio kabisa.
 
Mimi ni mkazi wa Nyasaka, kata ya kawekamo, wilaya ya Ilemela, Mkoa wa Mwanza.

Kero yangu kubwa ni wimbi la kelele zilizopitiliza kwenye makazi ya watu zinatoka kwenye nyumba za ibada, sehemu za starehe na wafanya promotion za biashara na makazi ya watu wanapofanya sherehe za harusi.

Imekuwa ni kawaida sasa kwa maeneo mbalimbali ya wilaya za Nyamagana na Ilemela (Mwanza) kukuta kuna uchafuzi mkubwa wa kelele katika makazi ya watu.

Jambo hili limekuwa sugu licha ya kwamba kuna sheria zimetungwa kudhibiti kelele na mitetemo na pia kuna mamlaka zimepewa jukumu hilo la kufatilia na kudhibiti kelele ila ni kama wamelala na hawajishugulishi nalo kabisa, wananchi ndio tumekuwa wahanga wa kelele hizi.

Serikali za Mtaa kuanzia mwenyekiti wa mtaa ambaye ndio mtu wa kwanza kudhibiti kelele wamekuwa hawajishughulishi na jambo hilo, ofisi za kata, Idara ya mazingira, Halmashauri ya Ilemela na Baraza la taifa la mazingira (NEMC) nao wamekaa tu maofisini huku mtaani wananchi tukikosa utulivu tokana na kelele zilizopitiliza kwenye makazi ya watu.

Mfano eneo nalokaa mie la Nyasaka msumbiji kuna kanisa la walokoke linaitwa Bethel linapiga muziki karibia kila siku kuanzia Jumatatu mpk Jumapili. Jumamosi wanapiga muziki kuanzia saa tatu asubui mpk saa tatu usiku hata kama hakuna watu kanisani, wanachofanya ni kuunganisha simu kwenye spika kisha wanafungulia sauti kubwa.

Wauza vilevi/pombe nao wakiamua weekend nzima kuanzia saa moja ni mziki mnene, hapo bado hawajaja watu wa promotion kutangaza bidhaa zao.

Pia mtu ana sherehe kwake anafunga mziki mnene usiku mzima hata siku mbili bila kujali watoto,wagonjwa,wazee na majirani wanaohitaji utulivu ili wapumzike.

Kero hii ya kelele imefanya tuchelewe kurudi majumbani kwetu ilimradi tukute washazima mziki. Siku za kupumzika nyumbani ni kero tupu zitokanazo na kelele.

Natoa wito kwa serikali na taasisi zake waliopewa dhima ya kuzuia uchafuzi huu wa kelele watimize majukumu yao,kwan kelele hizi zina athari kubwa kiafya na kijamii pia. NEMC NA OR TAMISEMI ni muda sasa wakachukua hatua na kusimamia sheria dhidi ya kelele hizi.
Na bahati mbaya zaidi miziki hupigwa kwa wingi siku za mapumziko, yaani unarudi mapumziko nyumbani unakutana na kelele za miziki kwenye majumba ya starehe, hii kero iangaliwe kama kero nyingine za uchafuzi wa mazingira.
 
Sijaona mahali ambapo misikiti imetajwa maana Hao ndio vinara wakelele wameweka mpaka vipaza sauti
 
Back
Top Bottom