NEMC, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa yahamasisha usafi wa mazingira na urejelezaji taka

NEMC, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa yahamasisha usafi wa mazingira na urejelezaji taka

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
Dar: NEMC na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Wafanya Usafi Ilala
IMG-20250111-WA0038.jpg

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeshiriki katika zoezi la kufanya usafi wa Mazingira lililofanyika katika Wilaya ya Ilala.

NEMC imeshiriki zoezi hilo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhamasisha wananchi kusafisha na kutunza Mazingira katika maeneo yao.

Zoezi hilo limeongozwa na Mkuu wa Mkoa mwenyewe, Mhe. Albert John Chalamila akiambatana Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo, Mkurugenzi wa Jiji, pamoja na watumishi wa Mkoa na Jiji la Dar es Salaam.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesisitiza uboreshwaji wa miundombinu ya ukusanyaji na utunzaji taka katika maeneo maalumu ili kutengeneza mbolea na nishati jambo litakaloongeza fursa za ajira pamoja na usafi wa Mazingira ili Jiji la Dar es Salaam liendee kuwa safi na kivutio kwa uwekezaji na utalii.

Washiriki wengine wa zoezi hilo ni pamoja na DAWASA, TANESCO na wafanyabiashara wa maeneo ya Wilaya ya Ilala.
IMG-20250111-WA0034.jpg
IMG-20250111-WA0035.jpg
IMG-20250111-WA0037.jpg
 
Hongera kwa Wakandarasi Kajenjere, Satek na Wagesa...hakika kazi yenu ilionekana
 
Back
Top Bottom