NEMC watoe mawasiliano ya kiofisi public wapewe taarifa nyingi kuhusu sehemu zenye uchafuzI wa mazingira uliokithiri

NEMC watoe mawasiliano ya kiofisi public wapewe taarifa nyingi kuhusu sehemu zenye uchafuzI wa mazingira uliokithiri

DodomaTZ

Member
Joined
May 20, 2022
Posts
84
Reaction score
118
Kazi nzuri ambayo inafanywa na Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) inatakiwa kuwa na mwendelezo.

Uwepo wao umekuwepo kwa muda lakini yawezekana hawajasikika muda mrefu kwa kuwa hawakuwa wameamua kuonesha majkumu yao hasa katika kulinda mazingira ni yapi.

Hivi karibuni jina la NEMC limeonekana na kusika kwa nguvu kubwa kutokana na kuchukua hatua ya kufungia baadhi ya sehemu za starehe ambazo zimekuwa zikichafua mazingira kwa kelele.

Binafsi nawashauri NEMC waweke namba za simu za kikosi kazi chao au njia nyingine zozote za mawasiliano ya kiofisi ambazo wananchi wa kawaida tunaweza kutoa malalamiko yetu.

Lengo ni kufikisha taarifa zaidia kuhusu maeneo mengi zaidi yenye changamoto ya kelele, naungana hoja ya kwa mchakato wanaoendelea nao wapo sahihi.




Lakini nitoe angalizo namba hizo kuna watu wanaweza kutumia vibaya kwa kuwachongea wengine kwa maslahi binafsi au chuki, hivyo kukiwa na utaratibu wa NEMC kutoa mawasiliano yao kuwe pia na kawaida ya wao kufanya utafiti au uchunguzi kabla ya kuchukua hatua.

Kongore kwa NEMC, endeleeni kusafisha njia lakini iwe kwa weledi uliotukuka ili msiwape nafasi wanaowapinga kuwatoa kwenye mstari.
 
Sambamba na namba waweke app ambayo mtu anaweza kutuma taarifa kwenye mfumo wao ikionesha location zilipo kelele bila kuexpose taarifa za informer,

NEMC inaweza kujiendesha bila ruzuku toka serikalini kaa kutoza fine kubwa kwa hao wachafuzi wa kelele na mitetemo, hivi sasa kuna maeneo mengi vichochoroni yenye kelele za muziki na machine za kugonga matofari pamoja na kunoa vyuma
 
Back
Top Bottom