Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Baraza la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (Nemc) limepiga marufuku uanzishwaji holela wa madampo mitaani na mabondeni na watu wanaodai kukabiliana na mafuriko yanayotokea wakati wa mvua.
Kwa mujibu wa Nemc madampo hayo holela yamekuwa yakihatarisha afya za wakazi waliyo jirani na maeneo husika na kuharibu mazingira.
Baraza hilo pia limezitaka halmashauri kutoruhusu uanzishwaji wa madampo hayo bila kuwa na utaratibu maalum ambao utapitiwa na wataalam wa Nemc kabla ya kuanza kutumika.
Uamuzi huo ulitolewa jana Mei 15 na Mkurugenzi Mkuu wa baraza hilo, Dk Samuel Gwamaka na alipofanya ziara ya kushtukiza katika mtaa wa Amani uliopo kata ya Mbezi juu jijini Dar es Salaam, baada ya kupata taarifa ya uwepo wa dampo katikati ya makazi ya watu.
Dk Gwamaka aliweka kambi kwenye eneo hilo akiwa na maofisa wa Nemc sambamba na polisi na baada ya muda mfupi magari ya taka yakaanza kuwasili kwa ajili ya kumwaga takataka.
Baada ya kuwahoji wenye magari hao walieleza kuwa wana maelekezo ya kumwaga taka katika eneo hilo baada ya kuwepo makubaliano kati ya wakazi na halmashauri ya Kinondoni.
Dk Gwamaka ameeleza kuwa ni kosa kwa halmashauri kukubaliana na wananchi kuanzisha dampo bila kuwa na utaratibu unaoeleweka ambao utawasilishwa na kupitishwa na Nemc ambao ndio wasimamizi wa mazingira.
Chanzo: Mwananchi