LGE2024 Nenda kajiandikishe

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

o_2

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2017
Posts
428
Reaction score
385
Juzi nilienda kujiandikisha kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Ni muhimu kama kijana kuhakikisha unatumia haki yako ya msingi kumchagua kiongozi bora anayemtaka atakaye hakikisha maendeleo ya jamii na nchi kwa ujumla.

Kulalamika mwisho 2024.
 
Bro utapoteza haki yako ya msingi. Kesho utalalamika.
 
Nini kinahitajika kujiandikisha?
Uwe na kitambulisho chochote. Cha mpiga kura kama uliwahi kuwa nacho, ila Ukiwa na kitambulisho cha taifa (NIDA) basi kazi itakuwa nyepesi zaidi.

Majina yako matatu, umri. Shughuli inachukua dakika mbili. Usikose mtu wangu. Tumia haki yako ya msingi.
 
Kama sina kitambulisho chochote?
 
Kuna mahali nilikuwa naongea na vijana,wanasema hali ya mwaka 2020 bado haijawatoka vichwani mwao wanaona kupiga kura ni kupoteza muda wao,mchakato wa kuoata wagobea wenyewe ndani ya vyama haukua wa kidemcrasia ,wanachama wanampitisha X uongozi unamuweka Y kugombe.Pia zile tuhuma za wizi wa kura. Labda kupata vitambulisho kwa ajili ya dhamana maana wanakamatwa kamatwa na polisi wanaulizwagqa vitambuliaho ili kutolea dhamana.

My take.Elimu ya uraia uongezwe nguvu.
 
Jina na umri βœ…
 
Mambo hayo hayapaswi kutukatisha tamaa. Tukiwa wengi, na nguvu inakuwa kubwa. Tuendelee kuelimishana kuhusu mambo haya.
 
Umejiandikisha kweli??? Mbona hakihitajiki chochote zaidi ya majina matatu na umri....
 
Kupotezeana muda tu. Tume ya uchaguzi isimamie chaguzi zote nchini kwa kitambulisho cha mpiga kura au NIDA. Hizi sarakasi za CCM hazina maana yoyote, TAMISEMI wafanye majukumu yao, viongozi wachaguliwe kwa usimamizi wa tume ya UCHAGUZI.
 
Reactions: o_2
Kupotezeana muda tu. Tume ya uchaguzi isimamie chaguzi zote nchini kwa kitambulisho cha mpiga kura au NIDA. Hizi sarakasi za CCM hazina maana yoyote, TAMISEMI wafanye majukumu yao, viongozi wachaguliwe kwa usimamizi wa tume ya UCHAGUZI.
Hii inafanyika kwasababu watu wanahama, wanakufa....lazima daftari liboreshwe. Lihuishwe ili taarifa sahihi za mpiga kura zipatikane. Narudia tena. Ni zoezi la dakika mbili tu. Kisha unaendelea na shughuli zako ukisubiri tarehe ya kupiga kura.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…