NENEO GANI SAHIHI? Ugali au Ugari

NENEO GANI SAHIHI? Ugali au Ugari

kimanuamanua

Member
Joined
Sep 25, 2013
Posts
80
Reaction score
15
Muda mrefu nimekuwa nikipata shida kutambua ni neno gani hasa sahihi kati ya

1. Ugali na Ugari...utamsikia mtu akisema "nina songa ugari", je ni sahihi
2. Kulowa na Kurowa...utamsikia mtu akisema "amelowa chapachapa", je ni sahihi
3. Mwango na Mlango
4. Mwizi na Mwivi

Basi kuna maneno mengi ambayo yanafanana na hayo na yamo ndani ya jamii zetu na hutumiwa na watu ambao hujigamba kuwa wao ni waswahili, sasa sisi ambao Kiswahili ni lugha ya darasani tushike lipi??

Wadau tupeni mwongozo
 
1.Ni ugali

2.Kulowa

3.. Sijui ulikusudia nini lakini mlango ndiyo kiswahili sahihi

4. Mwizi

Mwisho vitu vidogo kama hivi unatakiwa kuvijua na si kuja kupoteza muda humu JF.
 
Back
Top Bottom