Neno 'kashifu' linavyotumiwa na Wakenya ni sawa ?

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2006
Posts
4,191
Reaction score
677
mara nyingi nimekua nikifatilia habari kwenye vyombo vya habari vya kenya na hata BBC wakihariri habari wakenya hulitumia neno KUKASHIFU kama kulalamika au kupinga maamuzi au maneno yaliofanywa na wengine ntatoa mfano wa habari ilioripotiwa na BBC jana

Mshambulizi wa Uholanzi Arjen Robben amekiri kuwa alidanganya timu yake ikapewa penalti ya ushindi lakini akasema alikuwa ametegwa .
Kocha wa Mexico Miguel Herrera amemkashifu refarii wa mechi yao na Uholanzi Pedro Proenca kwa kuipendelea Uholanzi
.

hapa anamaanisha akipingana na maamuzi ya refarii. mm hunipa tabu maana nnavyojua mm kwa kiswahili cha zanzibar nilipotoka sina hakika ni Tanzania yote neno kashfa hutumika kwa dhamira ya matusi au matendo maovu na sio kulalamikia au kukosoa

nnaomba tusaidiane kuelimishana huenda mm sijaelewa vyema
 
mara nyingi nimekua nikifatilia habari kwenye vyombo vya habari vya kenya na hata BBC wakihariri habari wakenya hulitumia neno KUKASHIFU kama kulalamika au kupinga maamuzi au maneno yaliofanywa na wengine ntatoa mfano wa habari ilioripotiwa na BBC jana

.

hapa anamaanisha akipingana na maamuzi ya refarii. mm hunipa tabu maana nnavyojua mm kwa kiswahili cha zanzibar nilipotoka sina hakika ni Tanzania yote neno kashfa hutumika kwa dhamira ya matusi au matendo maovu na sio kulalamikia au kukosoa

nnaomba tusaidiane kuelimishana huenda mm sijaelewa vyema

Unauliza kuhusu kashfa au kashifu?

Kashfa ni Scandal
Kashifu ni Condem
 
Acheni kuumauma maneno! Jibu ni kwamba wanakosea kulitumia hili neno kashifu, kashifu haina maana ya kulalamika! Kocha alimlalamikia refa, wao wanasema alimkashifu, kukashifu ni kumsema vibaya mtu, aghalabu kumtukana na kumdhalilisha kwa kumtolea maneno mabaya!
 
Haswa,umemaliza yote.
 
Kosa waanlofanya watumiaji wa Lugha wa Tanzania ni kudhani kuwa wanaosema Kiswahili kinyume na wao wanakosea. KAtika IsimuJamii (social linguistics) hatuiti makosa, bali tofauti. Zaweza kuwa za kimaeneo, kihadhi na kadhalika.
 
Bado umemumusa maneno ndugu.
Nikweli kwamba huwa inatokea kunakuwa na tofauti katika matamshi nk, kwa hiyo kutofautiana kupo, ila haimaanishi kila anetofautiana na wewe basi yuko sawa eti kwasababu kule aliko ndivyo wanavyofanya.

Haiwezekani mtu atumie maneno mahala ambapo si pake, halafu ionekane ni sahihi eti kisa ndivyo walivyozoea! Ingekuwa ni rahisi hivyo kusingekuwa na haja ya usanifishaji wa lugha, na kila mpangilio ungekuwa sahihi!
 
Lugha kusanifishwa hakuwanyimi haki watumiaji wengine ambao lugha yao si sanifu kutumia lugha wanavyotaka, usanifu una tofauti na ufasaha. Nani anayepanga kipimo cha ufasaha ikiwa lugha zetu wote hazijasanifishwa, huoni walakini hapo?
 
Kosa waanlofanya watumiaji wa Lugha wa Tanzania ni kudhani kuwa wanaosema Kiswahili kinyume na wao wanakosea. KAtika IsimuJamii (social linguistics) hatuiti makosa, bali tofauti. Zaweza kuwa za kimaeneo, kihadhi na kadhalika.
Mkuu uko sawa lakini kwa muktadha wa neno hilo watakuwa wamekosea, hiyo habari inaonekana imetafsiriwa, ingeandikwa kwa kiswahili toka awali asingetamka hivyo. Condemn atakuwa sawa lakini sio kukashifu.
 
Back
Top Bottom