Neno 'kondakta' lilitoka wapi?

Neno 'kondakta' lilitoka wapi?

kindege534

Member
Joined
Jul 28, 2014
Posts
97
Reaction score
24
Habari za muda huu,
Nimejiuliza bila kupata majibu kwamba jina hili "kondakta" tunalotumia kwenye usafiri wa umma, chanzo chake au asili yake ni lugha gani? Nimewaza kwamba limetoka kwenye kiingereza "conductor" lakini nikaona kama mantiki haziendani.
Hapa ndio JF naomba kufahamu neno hili.
 
Mleta mada,jibidiishe kupambanua,kutofautisha na kuweka matumizi ya wakati wa maneno.
 
Nilicholenga hasa kufahamu ni asili ya neno na matumizi yake. Kamusi pia zinataja kwamba hawa bus fare collectors , choir leaders wanaitwa conductors.
Kwa elimu yangu ndogo waongoza kwaya wakipewa jina la conductors naweza kuelewa na nakubali kwa sababu bila wao uimbaji hauwezi kufanyika. Mambo ya sauti kupanda na kushuka n.k wao ndio madereva wa kwaya. Ukiwaita conductors inaleta mantiki.
Kwenye daladala jina 'collectors' ndio linaendana na uhalisia.
 
maneno ya conduct na collect ni tofauti kabisa.

Ku-collect ni kusanya vitu tu.

Ku-conduct ni kuelekeza watu au vitu ili zifanye kazi bila shida. Kwa hivyo conductor ni mtu anayeshugulikia daladala ifanye kazi au mtu anayeshugulikia choir ifanye muziki poa. Lakini kumbuka: ni kazi kidogo ya kuelekeza tabia sio kazi ya kudhibiti kabisa ama kuongoza ama kuendesha.
 
Back
Top Bottom