Neno Kongano

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258
NENO kongano limekuwa likisikika masikioni mwa baadhi ya Watanzania, ingawa huenda limekuwa likikanganya na kuacha maswali mengi kuhusu maana yake halisi.




Huenda kuna ambao wanalichanganya neno hili kongano na neno jingine kongamano ambalo pia limekuwa likisikika mara kwa mara.



Kongano, ni neno linaloeleza mkusanyiko wa wajasiriamali katika eneo fulani wenye madhumuni yanayofanana na ambao wanafanya biashara zinazofanana.



Biashara hizi zinawaunganisha watu hawa kukamilisha mnyororo wa thamani. Kwa maneno mengine kongano ni mkusanyiko wa watu au vikundi vya ujasiriamali au kampuni ambazo hufanya kazi kwa kushirikiana na kushindana.



Mpango wa Maendeleo ya Kongano ni wa Dunia ulioasisiwa nchini mwaka 2003, ulifaniishwa na wawakilishi wa Tanzania waliohudhuria semina inayohusu kongano iliyofanyika Sweeden.

Wawakilishi hao waliporejea nchini waliona umuhimu wa kuanzisha kongano zitakazoleta chachu ya maendeleo katika sekta binafsi. Mwaka 2005, mafunzo kuhusu kongano yalianzishwa rasmi.

Ili kongano iweze kufanikiwa kunahitajika uwepo ushirikiano wa wanataaluma,sekta binafsi na serikali.Ushirikiano wa wanataaluma,

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…