Neno 'Kupiga' halina mbadala?

Neno 'Kupiga' halina mbadala?

goukun wadey

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2020
Posts
241
Reaction score
284
Wanalugha naomba kujua ikiwa neno hili Kupiga haliwezi kupata usaidizi au lipo neno lingine lifaalo kwa ajili ya kusaidia neno hilo. Utasikia
  • Kupiga deki,
  • kupiga mswaki,
  • kupiga kura,
  • kupiga chafya,
  • kupiga chapa,

Hili neno kwanza tafsiri yake sio ya heri bali shari. Kwa hiyo ingependeza kama tungepata neno lingine litumike badala yake.
 
kupiga deki -- kunafisha, unafishaji

kupiga mswaki -- kusawisha, ukoshaji au kukosha (meno)

kupiga kura -- kudahini, udainishaji

kupiga chafya -- hekemua

kupiga chapa -- kuhatini, kuhatisha, uhatishaji

kupiga mbizi -- kukauni, kauni (mbizi)

kupiga msasa -- kusaniwiri, usaniwirishaji

kupiga dili -- tafirisha, utafirishaji

kupiga hodi -- kubisha hodi, adihini, hodisha

kupiga domo -- bwabwaja
 
Asante mkuu, naongezea; kupiga soga, kupiga ngoma, kupiga ramli, kupiga zumari, kupiga mfano.
 
Naona halina mbadala huwezi kisema kuchapa kura,kuchapa deki
 
basi tuseme

chapa kura

chapa deki

chapa mswaki

chapa chafya

bamiza chapa
 
Wanalugha naomba kujua ikiwa neno hili Kupiga haliwezi kupata usaidizi au lipo neno lingine lifaalo kwa ajili ya kusaidia neno hilo. Utasikia
  • Kupiga deki,
  • kupiga mswaki,
  • kupiga kura,
  • kupiga chafya,
  • kupiga chapa,

Hili neno kwanza tafsiri yake sio ya heri bali shari. Kwa hiyo ingependeza kama tungepata neno lingine litumike badala yake.
Vipi
  • nadeki, kudeki
  • naswaki, kuswaki
  • kuchapisha
 
Kupiga ni kutenda ama kufanya tukio..
 
Back
Top Bottom