Neno kutoka ISAYA 11

Neno kutoka ISAYA 11

jingalao

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
36,197
Reaction score
29,717
Ufalme wa amani

1 Kutatokea chipukizi katika kisiki cha Yese,

tawi litachipua mizizini mwake.

2Roho ya Mwenyezi-Mungu itakaa kwake,

roho ya hekima na maarifa,

roho ya shauri jema na nguvu,

roho ya ujuzi na ya kumcha Mwenyezi-Mungu.

3Atafurahia kumcha Mwenyezi-Mungu.

Hatahukumu kadiri ya mambo ya njenje,

wala kuamua kufuatana na yale anayosikia.

4 Atawapatia haki watu maskini,

atawaamulia sawasawa wanyonge nchini.

Kwa neno lake ataiadhibu dunia,

kwa tamko lake atawaua waovu.

5 Haki itakuwa kama mkanda wa kujifunga,

uaminifu utakaa naye kama mkanda kiunoni.

6 Mbwamwitu ataishi pamoja na mwanakondoo,

chui watapumzika pamoja na mwanambuzi.

Ndama na wanasimba watakula pamoja,

na mtoto mdogo atawaongoza.

7Ngombe na dubu watakula pamoja,

ndama wao watapumzika pamoja;

na simba atakula majani kama ng'ombe.

8Mtoto mchanga atacheza kwenye shimo la nyoka

mtoto ataweza kutia mkono shimoni mwa nyoka wa sumu.

9 Katika mlima mtakatifu wa Mungu

hakutakuwa na madhara wala uharibifu.

Maana kumjua Mwenyezi-Mungu kutaenea pote nchini,

kama vile maji yajaavyo baharini.

Walio uhamishoni watarudi

10 Siku ile chipukizi wa Yese atakuwa ishara kwa mataifa; mataifa yatamtafuta na makazi yake yatatukuka. 11Siku hiyo, Bwana ataunyosha mkono wake tena kuwarejesha watu wake waliosalia huko Ashuru, Misri, Pathrosi, Kushi, Elamu, Shinari, Hamathi na sehemu za pwani.

12Naye atatweka bendera kuwaashiria mataifa,

kuwakusanya Waisraeli waliodharauliwa,

kuwaleta pamoja watu wa Yuda waliotawanywa,

na kuwarudisha toka pembe nne za dunia.

13Wivu wa Efraimu juu ya Yuda utakoma,

hakutakuwa tena na uadui kati ya Yuda na Efraimu.

14Wote pamoja watawavamia Wafilisti walio magharibi,

pamoja watawapora watu wakaao mashariki.

Watawashinda Waedomu na Wamoabu,

nao Waamoni watawatii.

15Mwenyezi-Mungu atakausha ghuba ya bahari ya Shamu,

kwa pumzi yake ichomayo atakausha mto Eufrate,

nao utagawanyika katika vijito saba,

watu wavuke humo miguu mikavu.

16Tena, kutakuwa na barabara kuu toka Ashuru

kwa ajili ya watu wake waliobaki humo

kama ilivyokuwa kwa Waisraeli

wakati walipotoka nchini Misri.
 
Mmeanza kusujudu??, Tulipokuwa tunawaambia magufuli alipendwa na kutukuzwa na kakikundi kado Tena bahati mbaya wote wakakutana hawa maarifa, wakaishia kutumia miguvuu haya watoto wa mjini wakampiga KO ya maana. Saiz vimalikia vyake mtufu mnalialia hovyoo.

Samia kazi hapohapo ili tuelewana na hawa timu Burigi fc.
 
Mmeanza kusujudu??, Tulipokuwa tunawaambia magufuli alipendwa na kutukuzwa na kakikundi kado Tena bahati mbaya wote wakakutana hawa maarifa, wakaishia kutumia miguvuu haya watoto wa mjini wakampiga KO ya maana. Saiz vimalikia vyake mtufu mnalialia hovyoo.

Samia kazi hapohapo ili tuelewana na hawa timu Burigi fc.
soma vyema maandiko
 
Wote kwa pamoja watawavamia wafilisti walio magharibi.... Naam! Ubeberu utakomeshwa
 
Back
Top Bottom