Neno la leo: Kutoka mtaani kwetu

Neno la leo: Kutoka mtaani kwetu

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,319
Malonyalonya

Nguo za mtumba ambazo huuzwa katika furushi la jumla na kwa bei moja bila kujali ukubwa au aina ya nguo. Nguo hizi mara nyingi huhitaji marekebisho ya vipimo ili yaendane n aumbo la mvaaji, nguo za kike ndio hasa hupatikana katika kusanyiko hili.

Masoko maarufu kwa bidhaa ya aina hii ni pamoja na Tandale, Ilala, Tandika na Buguruni

Asili yake inaweza kuwa ile hali ya kuonekana kama bidhaa sisizo na thamani, mara nyingi humwagwa chini au kwenye meza kubwa.

NB; Kama unafahamu zaidi kuhusu msamiati huu, unaweza kuongeza yako.
 
Kachala...neno hilo pia hutumka kumaanisha "Msimela".
 
Katika maneno mapya yaliyowika 2012 nililipenda saana "Mburula", nilipenda pamoja na wimbo wao hao vijana waliofanya nijue Mburula ni nini...
 
Kwani '' mburula'' ni nani hasa? Je ni neno halali la kiswahili?
 
Mie naelewa ni neno la mtaani... Au nachemka?

So far nielewavyo Mburula ni mtu ambae anajifanya yupo juu sana kwa kujipaisha tofauti na ukweli halisi AMA mtu kujipa sifa hasa za kujikweza na hali siyo kweli. Tokana na wimbo na video atleast ndio nilielewa hivyo.
 
Back
Top Bottom