Neno lihusulo wajane. Usiseme hujaambiwa!

Neno lihusulo wajane. Usiseme hujaambiwa!

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
1 Mzee usimkemee, bali umwonye kama baba; na vijana kama ndugu;

2 wanawake wazee kama mama; wanawake vijana kama ndugu wa kike; katika usafi wote.

3 Uwaheshimu wajane walio wajane kweli kweli.

4 Lakini mjane akiwa ana watoto au wajukuu, na wajifunze kwanza kuyatenda yaliyo wajibu wao kwa jamaa zao wenyewe, na kuwalipa wazazi wao. Kwa kuwa hili lakubalika mbele za Mungu.

5 Basi yeye aliye mjane kweli kweli, ameachwa peke yake, huyo amemwekea Mungu tumaini lake, naye hudumu katika maombi na sala mchana na usiku.

6 Bali, yeye asiyejizuia nafsi yake amekufa ingawa yu hai.

7 Mambo hayo pia uyaagize, ili wasiwe na lawama.

8 Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.

9 Mjane asiandikwe isipokuwa umri wake amepata miaka sitini; naye amekuwa mke wa mume mmoja;

10 naye ameshuhudiwa kwa matendo mema; ikiwa amelea watoto, ikiwa amekaribisha wageni, ikiwa amewaosha watakatifu miguu, ikiwa amewasaidia wateswao, ikiwa amefuata kwa bidii kila tendo jema.

11 Bali wajane walio vijana ukatae kuwaandika hao, maana, wakizidiwa na tamaa kinyume cha Kristo, wataka kuolewa;

12 nao wana hukumu kwa kuwa wameiacha imani yao ya kwanza.

13 Tena, pamoja na hayo, hujifunza kuwa wavivu, wakizunguka-zunguka nyumba kwa nyumba; wala si wavivu tu, lakini ni wachongezi na wadadisi, wakinena maneno yasiyowapasa.

14 Basi napenda wajane, ambao si wazee, waolewe, wazae watoto, wawe na madaraka ya nyumbani; ili wasimpe adui nafasi ya kulaumu.

15 Kwa maana wengine wamekwisha kugeuka na kumfuata Shetani.

16 Mwanamke aaminiye, akiwa ana wajane, na awasaidie mwenyewe, Kanisa lisilemewe; ili liwasaidie wale walio wajane kweli kweli.

17 Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha.

18 Kwa maana andiko lasema, Usimfunge kinywa ng’ombe apurapo nafaka. Na tena, Mtenda kazi astahili ujira wake.

19 Usikubali mashitaka juu ya mzee, ila kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu.

20 Wale wadumuo kutenda dhambi uwakemee mbele ya wote, ili na wengine waogope.

21 Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, na mbele za malaika wateule, uyatende hayo pasipo kuhukumu kwa haraka; usifanye neno lo lote kwa upendeleo.

22 Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usizishiriki dhambi za watu wengine. Ujilinde nafsi yako uwe safi.

23 Tokeya sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara.

24 Dhambi za watu wengine zi dhahiri, zatangulia kwenda hukumuni; wengine dhambi zao zawafuata.

25 Vivyo hivyo matendo yaliyo mazuri ya dhahiri; wala yale yasiyo dhahiri hayawezi kusitirika.
 
Mjane ye yote ambaye hajafikia umri wa miaka sitini na ambaye alikuwa mwaminifu kwa mumewe, asiwekwe kwenye orodha ya wajane.

Mjane anayestahili kuwekwa kwenye orodha hiyo lazima pia 10 awe mwenye sifa ya matendo mema, aliyewalea watoto wake vizuri, aliyekuwa mkarimu, aliyewaosha miguu watu wa Mungu, ali yewasaidia watu wenye taabu na aliyejitolea kufanya mema kwa kila njia.

11 Lakini wajane vijana usiwaweke kwenye orodha hiyo, maana tamaa zao za kimaumbile zikizidi kule kujitoa kwao kwa Kristo, watataka kuolewa tena.
 
Lakini wajane vijana usiwaweke kwenye orodha hiyo, maana tamaa zao za kimaumbile zikizidi kule kujitoa kwao kwa Kristo, watataka kuolewa tena.
 
Mjane ye yote ambaye hajafikia umri wa miaka sitini na ambaye alikuwa mwaminifu kwa mumewe, asiwekwe kwenye orodha ya wajane.

Mjane anayestahili kuwekwa kwenye orodha hiyo lazima pia 10 awe mwenye sifa ya matendo mema, aliyewalea watoto wake vizuri, aliyekuwa mkarimu, aliyewaosha miguu watu wa Mungu, ali yewasaidia watu wenye taabu na aliyejitolea kufanya mema kwa kila njia.

11 Lakini wajane vijana usiwaweke kwenye orodha hiyo, maana tamaa zao za kimaumbile zikizidi kule kujitoa kwao kwa Kristo, watataka kuolewa tena.
Kwani kamusi yetu ya kiswahili fasaha inanenaje juu ya neno Mjane lililo sambamba na neno Mgane kwa jinsia jirani, isije ikaonekana kama bibliani imekuja kutoa elimu mpya
 
Kwani kamusi yetu ya kiswahili fasaha inanenaje juu ya neno Mjane lililo sambamba na neno Mgane kwa jinsia jirani, isije ikaonekana kama bibliani imekuja kutoa elimu mpya
Mgane ni mwanaume
Mjane ni mwanamke.. Wagane sio maarufu sana kwakuwa hawafiwi wengi😭
 
Back
Top Bottom