Neno mhanga nini tafsiri halisi?

Sokoli

Senior Member
Joined
Apr 14, 2017
Posts
192
Reaction score
128
Mtu aliyenusurika na ajali ni sahihi kumuita "mhanga wa ajali"?
 
Kujitoa Mhanga ni Kitendo cha kutaka kufanikisha jambo au kupeleka Ujumbe Fulani kwa namna yoyote ikibidi hata kujitoa Uhai. Aidha waliojeruhiwa kwenye ajali wanaitwa Manusura!
 
1. Mhanga - mfikwa wa jambo/ mtu alie kubwa na jambo , ambalo kimsingi si jambo la heri , jambo lenye kuleta simanzi/masikitiko/karaha.

Mhanga - umoja , Wahanga - wingi.

Mf. Mhanga wa maafuriko.

2. Mhanga- kitendo chaku ujasiri kuhusu/ kwenye jambo flani.

Mf. Alijitoa mhanga kuhakikisha ana usema uovu unao wafanywa na wanakijiji.

Sijui nime cheza mle mle.
 
Kujitoa Mhanga ni Kitendo cha kutaka kufanikisha jambo au kupeleka Ujumbe Fulani kwa namna yoyote ikibidi hata kujitoa Uhai. Aidha waliojeruhiwa kwenye ajali wanaitwa Manusura!
Nadhani jibu hili ni sahihi zaidi,asante mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…