Neno Mka

Mgosi Mokiwa

Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
34
Reaction score
5
Jamani kwetu sie waja leo waondoka leo twasema MKAZA MJOMBA.Nimehamia hapa Dar neno hili silitamki eti ni matusi kwa sababu ya neno 'KAZA'

Napenda kueleza kuwa neno Mka maana yake mke wa na kwa hiyo mkaza mjomba ni mke wa mjomba.Hiki ndio kiswahili sanifu.Kwa mantiki hii watu wanabananga kiswahili kwa kumwita mke wa mjomba shangazi.
 
Naona umejisikia tu kupost kitu huu ujinga ukakujia kichwani huoni hata aibu wewe
 
Kwa hiyo ipi bora, kuita shangazi/mke wa mjomba au mkaza mjomba?
 
Ukiwa Tanga au ukiwa na Watanga wenzako si vibaya kutamka mkaza Mjomba.
Lakini mkiwa mchanganyiko na jamii nyingine ni vizuri ukatumia Mke Mjomba /Mke wa Mjomba/Shangazi.

Usiwe na hofu Kiswahili kina maneno mengi yenye asili ya Tanga mfano Bunge, Kurugenzi, Mwanagenzi.

Utani !!!! Wabwanga na Wandele tishikamane
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…