Nimetafakari kwa kina, nimeshindwa kutoa neno moja kwa Simba mla nyama.
Ila ushauri mpana wanaopaswa wautafakari siku za usoni.
Kosa kubwa la msingi walilofanya ni kumkubalia mbunifu wa jezi zao wanazotumia .
Hebu TUTAFAKARI PAMOJA ule ni ubunifu wenye MIKOSI badala ya kuwa SIMBA MLA NYAMA amekuwa SIMBA MJERUHIWA.
Alama za jezi zinaonesha tayari Simba ameingia uwanjani akiwa amejeruhiwa kwa makucha kifuani na tumboni.
Nini kinafuatia ni kuvuja damu nyingi na kufa . MBUNIFU huyu hafai NUKSI inaanzia hapo ndo maana WENZENU wameita MADERA.