Neno 'nimeibiwa'

Neno 'nimeibiwa'

Capt Nemo

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2015
Posts
1,445
Reaction score
680
Naombeni jinsi ya kutumia neno "nimeibiwa" katika sentensi mbili tofauti

nikimtuma mtu anibebee mzigo nitasema "nimebebewa...." je? nikimtuma mtu aibe kwa ajili yangu?

itatofautianaje na nikitaka kutoa taarifa kuwa kitu changu kimeibwa kwa kujitanguliza mimi katika sentensi kama subject?
 
Tungo za kiswahili zina kanuni zake, na kiima na kiarifu, pia kikundi nomino katika kiarifu huakisi ni nomino ipi inapaswa kutangulia.
Kwa mfao;
-Mzigo wako ndio ulioibwa basi utasema;
Mzigo wangu umeibiwa au Nimeibiwa mzigo wangu.
-Kama wewe umechukuliwa bila ridhaa yako.
Hautasema kuwa umeibiwa bali umetekwa.
-Na kama umeagiza mtu akiibie utasema
Juma ameiba chupa kwa niaba yangu.
NIMEJARIBU
 
Kama ameiba au kubeba kwa ajili yako utasema;
-Juma ameiba nguo kwa ajili yangu.
-Juma amenisaidia kubeba mzigo.
Katika kuondoa utata ipo dhana ya kuongeza mofimu huru au mofimu tegemezi katika au baada ya au kabla ya neno tata.
Kwa kusema hivyo unaweza kuondoa utata katika tungo zifuatazo:-
I. Ameua Simba.
II. Mama anaota.
 
Nenda kaibe...

Hapo tayari umeshamtuma akaibe.
 
Back
Top Bottom