Shangingi lilitokana na nengo "Shangigi" la Kimasai likiwa na maana ya mwanamke ambaye hajaolewa; hivyo yuko kwenye soko la wanaume. Lilipoingizwa kwenye lugha ya kiswahili lilikuwa na maana hiyo hiyo ya mwanamke ambaye "yuko huru" kwenye soko la wanaume, lakini likawa limelenga zaidi wale wanaotembea na wanaume mbalimbali. Kwa wanawake wa namna hiyo walikuwa na tabia ya kuwa na ma-ta-ko manene, basi yale magari ya Nissan Patrol yaliyotoka mwanozni mwa miaka ya tisini nayo yaliitwa shangingi kwa sababu ya muundo wake ambapo fenders zake katika maeneo ya matairi zilikuwa kubw kama ma-ta-ko ya mwanamke wa ina ya shangingi wakati huo. Ni kutokana na hiyo extension ya kwenye Nissan Patrol baadaye magari ya Toyota Landcriuiser nayo yakajumuishwa kuitwa mashangingi. Leo huenda linatumika kwa hayo ma-Landcruiser tu, kwani nadhani umaarufu wa Nissan Patrol umefifia sana.