Exaud J. Makyao
JF-Expert Member
- Nov 30, 2008
- 1,518
- 24
Shemeji ni mtu aliye na udugu wa damu wa kikaka ama kidada na mwanandoa mwenzio.
Yaani mfano ni Kaka ama Dada wa Mkeo ni Shemejio vilevile kwa Mwanamke ni Kaka ama Dada wa Mumewe (japo mara nyingine Dada wa Mume huitwa Wifi likiwa na maana hiyohiyo ya Shemeji ila ni maalum tu kwa wanawake wenyewe, mwanaume haitwi wifi katika hali yoyote ile). Siku hizi pia watu wamekuwa wakitumia neno shemeji kwa mtu wa kabila jingine aliyeolewa/owa na mtu wa kabila lake, imekuwa ikitumika.
MAHMOUD
Mbona watu wanaoitana shemeji wala hawana undugu wowote?
Hujawahi kusikia watu wa namna hii?
MAHMOUD
Mbona watu wanaoitana shemeji wala hawana undugu wowote?
Hujawahi kusikia watu wa namna hii?
Mkuu Exaud, jamii za kitanzania zinaishi kama ndugu. Mfano mimi na wewe kama tunafanya kazi pamoja, tunasoma pamoja, tunaishi mtaa mmoja, ama ni marafiki, basi tunakuwa kama ndugu hivyo mkeo namuita shemeji. Na hata wasichana wakiwa marafiki, hujiona kama ndugu, hivyo mme wa rafiki yake humuita shemeji japo si ndugu. Vilevile hata kama nafanya kazi na binti ambaye kaolewa, ama nasoma naye lakini hatuna undugu, mme wake nitamuita shemeji.
Shemeji kwa Mme ni ndugu wa Mke wenye cheo cha dada, kaka ama binamu. Na vile vile kwa Mke ni ndugu wa Mme wenye cheo cha kaka na mabinamu wanaume, ikija ndugu wa mme ambao ni wadada na mabinamu ambao ni wasichana jina shemeji hugeuka na kuwa Wifi.
Siku hizi pia watu wamekuwa wakitumia neno shemeji kwa mtu wa kabila jingine aliyeolewa/owa na mtu wa kabila lake, imekuwa ikitumika.
Watanzania tumezidi kukwepa ukweli. Badala ya kumwita mke wa rafiki yako jina lake ........tunaendekeza mambo ya kuitana shemeji . . . Shemeji ibaki kwa ndugu wa mke kwa upande wangu au ndugu zangu kwa mke wangu......Shida inakuwa pale ambapo ndugu anakuwa na uhusiano wa mbali ambao unahitaji kama dakika 5 kuulezea.