Neno uliloambiwa na unalikumbuka hadi leo na linakusaidia

Ukiisha na mwanamke, ishi naye kwa akili sana... marehem mzee wangu

Maagano yanaumiza sana (kufiwa, kusafiri mbali na uwapendao, kumaliza shule unapoagana na wenzako n.k).. ex wangu

Mhubiri 9:10.. mchungaji wangu
 
Nakumbuka mama alinambia hivi. VYAKO VYAKO NA WENZAKO, UKIVIPATA VYAKO PEKE AKO. kuna kesi ilitokezea kipindi nasoma na mama angu ni mwalimu wa hiyo skuli, ayo maneno mpaka leo yamo kichwani na nakua makini sana nnaposhirikiana na mtu kwenye ishu yoyote ile
 
Usidanganyike ushindi wa Yanga ni wa kitambo tu. Ubovu wa Yanga ulikuwepo, upo na utaendelea kuwepo ๐Ÿธ๐Ÿธ
 
Thanks all mlio reply, nimejifunza vingi Kw kusoma mlicho ambiwa na kukisikia pia [emoji120][emoji122][emoji122][emoji122]
 
"usimdharau usiyemjua mwanangu..ishi na watu vizuri watendee yaliyo mema..Mungu pekee ndiye mlipaji wa kila jema na baya"..Mama yna2
R I.p
Poleeeeh sana blood cc, [emoji24][emoji24]
 
Nilipokuwa mjinga na mbumbumbu, Kuna watu wawili kwa nyakati tofauti walinambia, walimwengu sio wema km ulivyo na udhaniavyo, halafu wao wakawa wa kwanza kunionyesha nini maana ya hiyo sentensi,, walinifundisha kutoamini mtu haraka haraka
 
"Mjuu wangu kama mwanamke ana elimu kubwa kukuzidi wewe, mali nyingi au ni mrembo kiasi cha kuonekana karibu mji mzima. USIMUOE"
BABU YANGU 2000
 
Nilipokuwa mdogo 5 yrs Nilikuwa entertainer , nilipenda ngonjera , mashairi , maigizo ,music ...
Basi ilikuwa ni kawaida kila maadhimisho ya sikukuu na mikaeli na watoto nitapewa nafasi nyingi za kucover ... Nimeshasoma mistari mingi Sana ya bible ila huu haujawahi nitoka....

MITHALI 22:9 - Mlee mtoto katika njia impasayo hatoiacha hata atakapokuwa mzee .
Nina miaka twenty something sasa sijawahi sahau kamwe.

Pia zaburi ya 23 tulikuwa tukiimba Sana nyumbani before any task .
 
Ish kama upo vtani, hakuna kumuonea huruma mtu. Kila ulie n adui wako uskae ukimuamini mtu......

Skuambiwa na mtu nmejikuta tu naish na hiyo kchwan mwangu.......๐Ÿ˜Ž๐Ÿ˜Ž๐Ÿ˜Ž๐Ÿ˜Ž
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ