Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,478
- 3,659
kusaga tunajua kitendo cha kuponda kitu kutoka hali yabisi/ugumu (mfano mahindi, mawe, n.k) kwenda katika hali ya unga unga. Tunatumia neno 'usagaji' zaidi kwenye kitendo cha kutengeneza unga wa mahindi kwa ajili ya mlo (ugali) ambao ni kati ya vyakula vikuu vya mtanzania. sasa neno usagaji linaponasibishwa na kitendo cha wanawake kufanya ngono ya jinsia moja ni upotofu wa lugha na udhalilishaji wa kiswahili. kwamba kiswahili kimwshindwa kitafuta neno lingine la hicho kitendo. Neno ambalo limerasimishwa kutumika kwenye vitendo hivyo vya ngono ya jinsia moja kwa wanawake.
Vyombo husika vikae na kufanyia hili kazi ili kuondoa ukakasi kwenye matumizi ya kila siku ya neno hili 'usagaji'
Vyombo husika vikae na kufanyia hili kazi ili kuondoa ukakasi kwenye matumizi ya kila siku ya neno hili 'usagaji'