Neno 'usagaji' liondolewe kwenye matumizi haya yasiyofaa

Neno 'usagaji' liondolewe kwenye matumizi haya yasiyofaa

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Posts
11,478
Reaction score
3,659
kusaga tunajua kitendo cha kuponda kitu kutoka hali yabisi/ugumu (mfano mahindi, mawe, n.k) kwenda katika hali ya unga unga. Tunatumia neno 'usagaji' zaidi kwenye kitendo cha kutengeneza unga wa mahindi kwa ajili ya mlo (ugali) ambao ni kati ya vyakula vikuu vya mtanzania. sasa neno usagaji linaponasibishwa na kitendo cha wanawake kufanya ngono ya jinsia moja ni upotofu wa lugha na udhalilishaji wa kiswahili. kwamba kiswahili kimwshindwa kitafuta neno lingine la hicho kitendo. Neno ambalo limerasimishwa kutumika kwenye vitendo hivyo vya ngono ya jinsia moja kwa wanawake.

Vyombo husika vikae na kufanyia hili kazi ili kuondoa ukakasi kwenye matumizi ya kila siku ya neno hili 'usagaji'
 
hii ni moja ya hoja dhaifu zaidi kuwahi kuiona humu JF.
Ileweke
1.yapo maneno yenye maana zaidi ya moja na matumizi ndio hutofautisha.
2.yapo maneno mengine ambayo yana maana zaidi ya moja yenye taswira kama neno la usagaji,je nayo yabadilishwe?Mfano neno SHOGA(1.rafiki 2.mtu anaetumia kinyume maumbile kulawitiwa)
HAPO SI KUANZA KUBADILISHA MANENO NI KUJUA KUTUMIA MANENO.
na kama ingekuwa hivi sijui hali ingekuwaje mana maneno ya namna hii ni mengi na yapo kwenye jaribu kila lugha na hata lugha zetu za makabila lakini hayaleti tabu mana matumizi yake yanaeleweka
 
Back
Top Bottom