NET Group walipowekeza TANESCO tulifaidika au tuliibiwa?

NET Group walipowekeza TANESCO tulifaidika au tuliibiwa?

MKWEAMINAZI

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2023
Posts
930
Reaction score
1,304
Wadau nawasalimu,

Suala la kudai eti kuwapa bandari hawa Waarabu wa DP World ili wawekeze sidhani kama tutakwepa kuibiwa.

Ni aibu kwa Serikali yenye vyombo vya kupambana na wizi leo kudai eti bandarini kuna majizi, mapato yanaibiwa.

Serikali inayoshindwa kuwadhibiti hao wezi ni Serikali dhaifu na kama Serikali inajua inaibiwa na wazi hata wezi inawajua, inashindwa nini kuwakamata au ndio kulindana?

Wakati wa utawala wa Rais Mkapa kulikuwa na Mwekezaji TANESCO alikuwa anaitwa NET Group kutoka Afrika Kusini. Kilichotupata Watanzania wote tunakijua mpaka NET Group alifukuzwa

Uwekezaji sio kuzuia Wizi na kuongeza Mapato, inaweza kuwa ni kuibiwa zaidi.

Mifumo mibovu ya uendeshaji bandari ndio chazo cha wizi bandarini.
 
Bongo kinachotugharimu ni Rushwa na ufisadi. Mamlaka zipo ila hazina guts za kuzuia sababu wanufaika ni hao hao mameneja na viongozi wa taifa.
 
Bongo kinachotugharimu ni Rushwa na ufisadi. Mamlaka zipo ila hazina guts za kuzuia sababu wanufaika ni hao hao mameneja na viongozi wa taifa.
Sio hao tu, hata ukiweka Mtaani dula la Mangi ukamtafuta kijana akakaa bado utaibiwa. Kwa kifupi watanzania sio waaminifu
 
Sio hao tu, hata ukiweka Mtaani dula la Mangi ukamtafuta kijana akakaa bado utaibiwa. Kwa kifupi watanzania sio waaminifu
Sasa nani ameasisi hilo? 🤣 Maana viongozi ndio vioo vya jamii. Taifa lenye viongozi wezi lazma raia wawe wezi.

Ukiweka restrictions na kiongozi aka potray image ya uadilifu itawapa moyo raia kujiona waadilifu. Sasa mtu anayekwambia wewe usiibe yeye anajenga magorofa kwa fedha za wizi na dili. Unaweza ukamzingatia hata kidogo?
 
Tuliibiwa, wote wanakuja kwa gia kamq hizo na takwimu za hapa na pale kuonesha namna uzalishaji utakavyo ingezeka, mwisho wa siku wanafanya lobbying na kutoa rushwa mambo yao yanapita kisha tunaibiwa.

Ni mambo ya fedheha kabisa kujirudiarudia, ifike mahali tuanze kunyonga watu wanaosababishia nchi hasara. Maana itakua miaka nenda miaka rudi wapumbavu wachache wanauza nchi kwa manufaa ya familia zao. Pumbavu sana.
 
Punguza kupotosha
Net group hawakuweza Tanesco
Net gruop waliletwa kuliandaa Tanesco kuuzwa na kugawanywa
JK aka cancel hiyo plan wakaondoka
 
Back
Top Bottom