Netanyahu autaka ulimwengu kuipinga ICC

Netanyahu autaka ulimwengu kuipinga ICC

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameutolea wito ulimwengu kuchukua hatua dhidi Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kabla ya kesi ya uhalifu wa kivita inayoweza kufunguliwa dhidi ya Israel.

Mwendesha mashtaka mkuu wa ICC Fatou Bensouda amesema mwezi uliopita kwamba kuna uwezekano wa kuanzishwa uchunguzi wa uhalifu wa kivita dhidi ya hatua za kijeshi za Israel katika Ukanda wa Gaza pamoja na ujenzi wa walowezi wa Kiyahudi katika Ukingo wa Magharibi.

Israel ambayo sio wanachama wa ICC, imesema mahakama hiyo haina mamlaka hayo na kumshutumu Bensouda kuwa na chuki dhidi ya Wayahudi.

Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Kikristo TBN, Netanyahu amemsifu rais wa Marekani Donald Trump kwa kuikosoa ICC na kuwataka viongozi wengine nao kufanya hivyo.
 
Netanyahu bana,wakati viongozi wa nchi zingine wanafunguliwa mashitaka alikua kimyaaa
 
Netanyhau amesahau madhira ya HITRA na unyama waliofanyiwa,sasa yeye ndio kageuka HITRA na hataki vyombo vya haki.
 
Huyu jamaa jina lake linanchekeshaga sijui kwa nini
 
Back
Top Bottom