Katika haya maisha kuna vitu huwa tunajiapiza hatuwezi kuvifanya kwasababu tunahisi sio hadhi zetu au vinatutia kinyaa lakini baadae tunabadili msimamo.
Baada ya kumaliza degree nilijiapiza sitakuja kufanya kazi zisizo za ofisini, msoto ulinisugua bila mafuta, njaa inauma, nilianza kusaka vibarua, kuna siku niliwahi kukimbia kazi tuliambiwa tuchimbe mashimo ya kuweka nguzo, unapiga sululu lakini wapi.
Niliapa sitakuja kupelekeshwa na mwanamke, Niliwahi kutana na binti kutoka nyanda za juu kusini aiseee !! nilikamatwa kichwa jamani, binti ana kiburi yule lakini alipokuwa akiniambia kama nahisi usumbufu tuachane namnyenyekea. nikiwa na wenzangu naji mwambafai vibaya mno 😀😀
Niliwahi kuapa siji kuwa mvutaji wa sogara, niliwadharau sana watu wanaovuta, one day kama masihara hivi nikatesti nione tu inavyokuwa, katabia kakajiendeleza nikakamatwa kisawa sawa hadi kuna kipindi navuta ilimradi tu maana sihisi chochote, kila nikiwa nataka kuacha koo linawaka moto linahitaji kupozwa na moshi, ilikuwa ni vita kali sana Mwili vs Nafsi, nashukuru niliacha ila haikuwa rahisi