1. Mitandao mechafuka,
Watu wanalalamika,
Machozi yanawatoka,
Sabaya wamemchoka,
2. Kila mtu ni Sabaya,
Wamsema kwa mabaya,
Sabaya kawa Sabaya,
Sabaya wamemchoka.
3. Mara wale kawaonea,
Hawa nao katufanyia,
Huyu nae namchukia,
Sabaya wamemchoka.
4. Sabaya hakamatiki,
Sabaya haonyeki,
Sabaya Hashauriki,
Sabaya wamemchoka.
5. Nilimsikia Mgwira,
Akimwonya kwa busara,
Sabaya akafura,
Sabaya wamemchoka.
6. Hivi kwanini Sabaya,
Kila mtu Sabaya,
Sabaya huoni haya?
Jina lako tumechoka.
7. Mitandao inasema,
Wewe mwingi wa dhuluma,
Unapokonya ndarama,
Jina lako tumechoka.
8. Cheo chako watumia,
Watu wako kubutua,
Watu unawaonea,
Jina lako tumechoka.
9. Nchi yetu ya amani,
Wainajisi kwanini?
Kwani wewe una nini?
Jina lako tumechoka.
10. Umekuwa mungu mtu,
Wajiona kila kitu,
Roho mbaya ina kutu,
Jina lako tumechoka.