Baada ya siku 1,550 (miaka minne na miezi mitatu) ya mateso gerezani hatimaye leo mahakama imemuachia huru mzee James Rugemalira. Alipewa mashtaka ya uhujumu uchumi na utakatishaji pesa. Akaambiwa akiri, alipe ili aachiwe huru. Mwenzake Harbinder Seth (Singasinga) baada ya kuteseka miaka minne jela akaamua kulipa, akaachiwa.
Lakini Rugemalira akakataa kukiri, na akakataa kulipa akidai ni kesi ya kubumba. Akasema sikuiba, nilifanya biashara halali na serikali. Nikalipwa malipo halali. Kama kulikua na tatizo kwenye mikataba waulizwe viongozi wa serikali walioandaa mikataba hiyo, si mimi.
Nachojua nilililipwa fedha halali, na nikatoa sehemu ya fedha hizo kuwapa marafiki zangu. Kwahiyo pesa zilikua zangu na niligawa changu. Akaambiwa mzee omba radhi usamehewe. Akasema siwezi kuomba radhi bila kufanya kosa.
Akaambiwa mwenzako "Singasinga" amekiri kosa na ameachiwa, wewe unaweza kufia jela. Akasema kama nitafia jela it's okay lakini nasimamia nachokiamini. Huo ndio umekua msimamo wake kwa siku zote 1,550 alizokaa jela. Leo DPP kamfutia kesi. Ameachiwa huru bila masharti yoyote. Hajaomba msamaha, hajalipa, hajakiri.
Martin Luther King Jr aliwahi "Stand for what is right, evenif that means standing alone" akimaanisha simama katika haki bila kuyumbishwa, hata kama utasimama peke yako." Na hicho ndicho alichokifanya mzee Ruge. #JusticePrevailed #HakiImeshinda [emoji123]
[\CODE]