New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

With this kind of myopic thinking of continuing being European economic satellites, Tanzania condemns herself into an economic ruin with zero chance of creating jobs, lowering taxes to the poor and boosting real incomes.


Do we ever learn?


More taxes burdened to the poor is a red flag that the economy is structured in a such a way to serve our colonial masters for a song. No wonder a debt burden is a noose hanging on our necks each one of us.


Those in the Treasury who deceives us that the debt burden is bearable ought to answer this question honestly...WHAT IS THE PERCENTAGE OF RECURRENT BUDGET SERVICE INTEREST RATE PAYMENTS PER ANNUM.

Anything more than 10% of recurrent budget to service foreign debt is SIMPLY UNACCEPTABLE for very obvious reasons.






Sent from my SM-A715F using JamiiForums mobile app
 
Dissecting axed RCs.



Habari ya mujini the comedian is back and JK strikes back at those who ridicule him during the evil hour of Mwendazake.



Can someone teach JK the value of forgiveness even without an apology? Babu Seya and son tested the limits and opportunities of his absolution brooking a huge disappointment only for Mwendazake to politically capitalize and pat them on a shoulder with a popular clemency!

It is in forgiveness of those at our mercy we know the peace of God dwells in us. Why lodge evil thoughts against your neighbour if really God rules your life? Easier said than done, of course. We love to exact revenge.....albeit we know revenge not our portion in this life but His alone! But do we really trust Him to do us justice? It is a question we seldom answer honestly.

Can Hapi look back and agonise his reckless remarks against the now putative leader?

" ......wastaafu wakae kimya......tuachie sisi tushughulike nao....." well wastaafu now have a last laugh at your agony, reckless boy.......waheshimu wazee inalipa kijana... it is scriptural, we must remind and emphasize!

Few will shed crocodile tears for Hapi except those dependent on his wherewithal, obviously.

Curiously, Kafulila who epitomized political hypocrisy has been shown the door. Difficult to glean the reason presuming he was not caught with his fingers inside the Covid-19 kitty...or donor benevolence which of lately has been gutted by unscrupulous presidential picks....(we have already covered this narrative somewhere else in this discourse.)


But it is the unexpected return of the comedian in chief who ace the latest news. We know he begged in private profusely amounting to intense lobbying.....for the vagaries of her mercies which are few and far in between, but, they are there albeit grudgingly we must acknowledge.


"Sitarudia mama......msinichukulie serious sina nia mbaya na wewe" could mropokaji remake himself with these grovelling tactics or.......he is about to take us into another comic roller-coaster that will leave our ribs in stitches but hurting those who trusted him?

.......my imagination may be extremely fertile but not necessarily truthful must humbly concede.....




Your browser is not able to display this video.


Sent from my SM-A715F using JamiiForums mobile app
 
SAKATA LA TEGETA ESCROW

Najua wengi wanalijua swala hili kwa juu juu kwa kuwa linazungumziwa kwa lugha ya kipigaji ya kitaalamu kiasi cha kuwatoa kwenye reli wanaotaka kulielewa sakata hili.

Makala yangu itajitahidi sana kuongelea hili sakata kwa lugha nyepesi ili wote tuelewe.

Picha linaanza kwa Kijana mmoja wa kamamo wa Kihaya kuacha kazi benki kuu ya Tanzania

Kijana huyu japo umri umesogea kidogo anajiunga chuo kikuu cha Dar Es salaam kama “mature student)

Kijana huyu analiza chuo kile kwa kuibuka na “First class” ya biashara.

Kijana huyu baadaye anakuwa mmoja wa shareholders kampuni ya kwanza ya mawasiliano Tritel.

Anamiliki shares kupitia kampuni yake ya VIP Engineering and Marketing

Huyu kijana ni mtu mwenye akili nyingi sana,

Ni bingwa wa lobbying na negotiations.

Enzi zile ukiwa na deal yako yako kubwa ya biashara ambayo inahitaji ushawishi basi isingekuwa ajabu kuelekezwa uonane na kijana huyu ili mambo yako yakunyookee.

Kama umeangalia series ya “The Godfather” basi si vibaya ukimuita kijana huyu “le Conciliale”

Baadaye mzee huyu kupitia kampuni yake ya VIPEM (VIP Engineering and Management) akaingia ubia na kampuni ya Malaysia iitwayo MECHMAR.

Wabia hawa wawili wakaanzisha kampuni ya IPTL iliyokuwa na nia ya kuiuzia serikali Umeme.

Katika ubia huu MECHMAR akawa anamiliki hisa kwa asilima 70 huku VIPEM akimiliki asilimia 30

Hapa nitawarudisha nyuma kidogo ili mjue Ruge aliingia vipi ubia na MECHMAR

Wakati Kampuni ya Mechmar inataka kuingia nchini kufanya biashara, ilihitaji mikopo kutoka benki ili kutumia kama mtaji wa kununulia mitambo ya kufua umeme.

Mazingira ya kupewa mikopo yalikuwa magumu kwani Mechmar hawakuwa wanamiliki ardhi yoyote Tanzania.

Hapa ndipo Ruge alipojipatia deal kwani yeye alitoa ardhi yake iliyopo Tegeta ili itumike kuwekea mitambo ya IPTL lakini kwa masharti amewe hisa asilimia 30.

Kwa hiyo Ruge akawekeza ardhi tu na sio pesa.

Mabenki mawili ya nchini Singapore yaliikopesha kampuni ya Malaysia iitwayo MECHMAR kiasi cha Usd milioni 100 iliyokuwa imepata tenda ya kutengeneza mtambo wa kufua umeme ya IPTL huko Tegeta Jijini Dar

Hapa unaelewa nini kwanza?

Nisome[emoji116]

Yaani mabenki mawili (Bumiputra Bank na Sime Bank) wanampa mkopo MECHIMAR ambaye anaenda kujenga mitambo ya IPTL


Unaona chain hiyo?

Yes ni chain hapo inaanza!

kwa kuwa hii IPTL nayo ni Kampuni

Zaidi ya yote hii ni kampuni yenye wabia wawili

So mkopo wa yale mapenki mawili ya Singapore umeenda kampuni ya Malaysia ya MECHMAR ili kwenda kujenga mitambo ya IPTL yenye wabia wawili ambao ni

MECHMAR wenyewe waliopewa mkopo.
VIP Engineering inayomilikiwa na James Rugemalila


Mwaka 2002 ikiwa ni miaka minane tangu kuanzishwa kwake ndipo kampuni hii ikaanza kuuza umeme.


Mwezi mmoja tu baada ya IPTL kuweka mambo yake sawa na kunza uzalishaji James Rugemalila ambaye ni mbia mdogo wa IPTL akamfungulia mshtaka ya madai bia mwenzake MECHMAR.

Malalamiko yake hasa yakiwa ni kutopokea gawio lake la 30% kwenye mtaji wa IPTL tangu kuanzishwa.

Hii ilikuwa kama “machale kundesa” au kushikwa na machale kwani Ruge hakuwa anajua lolote juu ya mkopo wa mabenki ambayo MECHMAR alisign kwa niaba ya IPTL

Ruge alishtuka zaidi mwaka 2005 baada ya benki ya Standard Chartered ya Hongkong kununua lile deni la yake mabenki mawili ya Singapore ikiwa ni miaka mitatu tangu aanze kudai gawio lake.

Yaani MECHMAR kama majority shareholder alikuwa anaingia mikopo kwa jina la IPTL hali hii ikaanza kumtia mshaka mzee wa kihaya hivyo akawa anataka kujua swala la gawio lake.

Akapeleka ombi mahakamani Kampuni yao ifungwe kila mtu afe na chake.

Wakati shauri hili lipo mahakamani, “Joka lenye makengeza” akiwa kama mwanasheria mkuu akafanikiwa kuyaona madai ya James,

Joka la makengez akamuita Mzee james na kumuuma sikio kuwa anaweza kupoteza kesi ile kirahisi sana kwani hana hajapima ardhi yake ya tegeta ilipo mitambo ya IPTL

Joka la makengeza alamshauri Ruge aondoe kwanza kesi kisha apime ardhi fasta.

Mzee wa Bcom First class akaelewa somo.

Akatoa kesi mahakamani

Akawageukia ardhi,

Kipindi hicho pale ardhi kuna “nshomile” wenzake kibao akiwemo Rutabanzibwa kama KM.

Waziri akiwa ni mama Tiba naye nshomile.


Wakati mzee ruge anapambana na hali yake, kwa upande mwingine Tanesco ikawa imegoma kuilipa IPTL pesa zake za “Capacity charges” ambazo zilikuwa zinatozwa kwenye kila unit ya umeme ambayo IPTL ilikuwa inaiuzia Tanesco.

Hii ilitokana na Tanesco kuanza kushtukia kuwa kiasi cha mtaji ambacho IPTL ilidai imewekeza si halisi.

Kiasi hiki cha mtaji ndio huwa kinatumika kukokotoa “capacity charges”

Kwa kuwa nchi ilikuwa kwenye uhitaji wa umeme ndipo ikaamuliwa IPTL iendelee na uzalishaji huku malipo yake yakiingizwa kwenye account maalumu ya Escrow pale BOT.

Malipo yangeendelea kama kawaida lakini yatakiwa chini ya BOT mpaka utakapotolewa utatuzi wa mgogoro ule.

Pesa ikazidi kuingia hadi kufikia kiasi cha Tshs bilioni 306.


Mate yakaanza kuwatoka wote walioijua akaunti hii.

Tuishie kwanza hapo kisha tuelekeze camera yetu upande mwingine.

Wakati kijana huyu anapiga mishe zake za kumletea ugali wake kihalali yeye na familia yake, upande mwingine kulikuwa na mtu mwingine anajitangazia Jamuhuri.

Naam

Upande mwingine kuna kijana mwingine mzaliwa wa Iringa mwenye asili ya Asia anapiga mitiksasi yake.

Kijana huyu maarufu kwa jina la singasinga akiwa na miaka 20 tu, anashirikiana na nduguze kufungua kampuni ya ujenzi ya Ruaha Concrete mwaka 1977.

Ndugu alioshirikiana nao kufungua kampuni hii ni Nota Singh na Manjit Singh.

Miaka ya 80 singasinga huyu akahamia nchini Kenya Jijini Nairobi kwa mshikaji wake aitwaye Gideon ambaye alikuwa ni mtoto wa rais wa Kenya Arap Moi.

Huko zinapigwa deals nyingi na Gideon huku Singa akiwekwa front.

Wakamiliki maapartment kibao Afrika kusini na Singa akitokea kwenye nyaraka za umiliki.

Baadaye kampuni yake ya Ujenzi ya Ruaha Concrete ikapewa kazi jijini Nairobi mwaka 1995 kujenga barabara za mitaa.

Mradi ulikuwa ni wa Kshs milioni 197 lakini pesa ikaongezwa mpaka Kshs milioni 570.

Hata hivyo wakati wa kukabidhi kazi mwaka 1998 kazi hii ilikataliwa kwa kuwa chini ya kiwango na kuibua kashfa kubwa.

Kashfa zilikuwa nyingi kule kenya na wala leo sio nia ya Uzi huu.

Sasa bwana, Huyu mshkaji akarudi bongo

Naam!

Alikuwa kanusa harufu ya pesa yatima zisizo na baba wa mama.

Jamaa lishajua kuwa kuna mgogoro baina ya Tanesco na Kampuni ya IPTL


Jamaa chaap akafungua kampuni ya kufua umeme ya Pan African Energy PAP


Kisha jamaa chaap akaingia Joint venture na kampuni ya Adhunik Group na wakanunua kitalu cha gesi na mafuta huko Mnazi bay Songo songo.

Katika hali isiyoeleweka mahusiano ya kimkataba baina ya Tanesco na Song Gas yakaanza kuteteleka baada ya Jamaa huyu kuja.

Ukafata uhuni mwingine,

Ilianza hivi,

Ile kampuni ya Malaysia ya MECHMAR ambayo imepokea mkopo toka benki za Singapore ikauza hisa zake katika soko la gizani.

Nasema la gizani kwani hakuna nyaraka yoyote iliyowekwa wazi kuonyesha manunuzi ya hisa toka kampuni moja hadi nyingine.

Kwanza iliuza hisa kwa kampuni ya Piperlink kisha ikaziuza hisa zake kwa PAP

So all over sudden Singa akawa anaimiliki IPTL na akarithi mitambo yenye uwezo wa kufua megawatts 100 bila kuingiza hata senti moja.

Yaani Ruge akajikuta anakuwa na Singasinga kama mbia mwenzake na sio Mechmar tena.

Baada ya kuundwa ubia huu kufatia mlolongo wa matukio,


Huu ndio wakati Singa akaanza kuyatolea macho mapesa yale na akataka kumzidi kete mbia mwenzake Ruge.

Sigh akataka asepe na pesa yote.

Ruge akaumwa sikio

Alichofanya Ruge ni kushirikiana na watu mbalimbali kuhakikisha anapata mgawo wake.

Akawauma sikio TRA kuwa kuna pesa pale BOT ambazo zinapaswa kukatwa kodi kwa kila mbia.

Yaani Ruge na Singa walipaswa kulipa kodi kwenye ile pesa hivyo katika ile pesa kulikuwa na pesa ya Serikali kwenye kodi.

Ruge akacheza na watu wote wa muhimu kama vile waziri wa nishati, mwanasheria wa serikali nk.

Katika maandalizi ya kupokea pesa zile ndipo Mzee Ruge akafungua akaunti katika benki ya Mkombozi.

Mabenki mengine ni kama yalikuwa yamenusa harufu ya “flaud” hivyo yalikataa kumfungulia akaunti mzee Ruge ili pesa zile zipitishiwe kwao.

Kwa kuwa Ruge alikuwa muumini na mtoa “zaka” mkubwa kanisani, aliweza kuwa karibu na maaskofu wa kanisa lake.

Maaskofu waliokuwa katika bodi ya wadhamini wa benki ya Mkombozi ndio waliomsaidia Ruge kufungua akaunti kwenye benki ya mkombozi.

Hapa ndipo unaona jinsi askofu Kilaini na Nzigirwa walivyoingia pichani kwenye hili sakata.

Basi ndio hivyo mchuzi ukaenda kutolewa

Pesa za Ruge zikapitia bank ya Mkombozi

Pesa za Singa zikapitia Stanbink bank

Ruge alipopata chake na kwa kuwa mzee sio zurumati akaanza kutoa Shukrani kwa wote waliomsaidia kupata pesa zake na kisha akalipa kodi iliyostahili TRA.


Ndio maana unaona watu walitumiwa miamala na Ruge kutokea benki ya Mkombozi.

Singasinga yeye ndio alifanya kufuru kabisa kwani ilibidi camera za bank ya Stanbinc zizimwe ili watu waweze kuondoka na pesa Cash kwenye magunia kwani hawakutaka ushaidi kupitia miamala ya kibenki.

Kwa hiyo utaona kwa upande fulani Ruge ndiye aliyeziamsha taasisi juu ya ufisadi uliotaka kufanywa na singh ingawa naye alikuwa ni mshirika wa ukwapuaji lakini akiwa amekwepa mianya yote ya kumsababishia kesi.

Sakata hili lilikuja kuibuliwa bungeni baadaye na Mbunge Kafulira hali iliyolazimu Bunge kuunda kamati kuchunguza swala lile.

Hii ndio ilisababisha mwanasheria mkuu wa serikali kumwita Kafurila Tumbiri bungeni.



Ripoti ya kamati ile ilisababisha Waziri tibaijuka kuachia ngazi kama waziri wa ardhi, Mwanasheria mkuu na wengie wakaachia ngazi pia.


Jinsi walivyokamatwa,

Ruge yeye kwake haikuwa tabu kwani alifatwa tu nyumbani kwake na kuchukuliwa.

Utata ulikuwa kwa Singasinga ambaye alishatonywa kuwa kuna mpango wa kumkamata.

Nanukuu,

“Unajua Singasinga alishajiwekea utamaduni wa “kukata posho” pale Airport kwa kila mtu either awe anaingia au kutoka”

“Ilikuwa ni rahisi sana kujia leo singasinga ataingia nchini au kutoka kwani anakuwa ameshatembeza “bakhshishi” muda mrefu kwa kutumia wapambe wake”

Kwa kawaida alikuwa anapitia VIP

Sasa Singa akawa ameshajua anatafutwa adakwe akawa anataka kuondoka kwenda kwenye makazi yake huko sandtown kwa Madiba.

Alishajuzwa kuwa jalada lake mkuu analala nalo na viatu

Siku ya Ijumaa tarehe 16/06/2017,Seth alikuwa aondoke na ndege ya shirika la ndege la South Africa,flight number SA187 inayotoka Dsm kuelekea Orival Reginald Tambo International Airport,iliyotarajiwa kuondoka saa 9 na dk 35 alasiri

Afrika Kusini ndiyo yalipo makazi ya Seth baada ya kupata mgogoro wa kifisadi na kupata shida ya kuishi Nairobi Kenya,alihamia huko Afrika Kusini.

Siku chache kabla ya siku ya kuondoka jamaa akatuma wapambe wapitishe rupia kwa watu wa Mingrationa, usalama, etc pale airport

Katika hali ya kushangaza mpunga wake watu wakakataa kuupokea na kuishia kusema “Ahsante”


Mpaka ijumaa asubuhi siki ya safari ngoma ilikuwa bila bila.

Sethi akaamua ngoja acheze kamali

Saa nane mchana akaonekana akiwa ameongozana na mwanamke mmoja Airport mpaka VIP Terminal II

Jamaa alakamilisha taratibu zote za “check in” akawa na boarding pass yake mkononi.

Kumbe wachawi tunamchora tu

“Taarifa zilishafika mahali husika,kuwa Singasinga yupo Airport tayari kwa safari,akiwa na "boarding pass" mkononi na muda wowote ataingia kwenye ndege tayari kwa safari.”

Bila kutarajia,wakati amevuka vihunzi vyote,akiwa anajongea kuingia katika gari la VIP,linalotumika kuwatoa wageni wa VIP eneo la VIP Lounge kuelekea kwenye ndege,ghafla ikatokea gari nyingine,kutoka mahali kusipoeleweka,likiwa limepitia mlango wa dharula na kusimama mkabala na lango la kutokea VIP lounge.

Palepale Harbinder akaamuliwa kuingia kwenye gari hilo lililokuwa na vioo vya giza,na kuachana na benzi la VIP VAN lenye maandishi ya kampuni ya Swissport kwa pembeni,mara moja gari ikageuzwa na kupelekwa kusikojulikana,mpaka mapema Jumatatu,Seth na Rugemalila walipoibukia mahakama ya Kisutu tayari kwa kusomewa mashitaka ya Escrow.


Tuliishia kuwaona wawili hawa mahakamani huku mmoja akiomba arudishe pesa na mwingine akikataa


Mmoja akarudisha pesa mmoja DPP akasema hana nia ya kumshitaki.


Wote sasa wako “kitaa”


MWISHO

Sent from my SM-A715F using JamiiForums mobile app
 
JINSI WANAFUNZI WA YESU KISTO WALIVYOKUFA.!

1. #Mathayo.
Huyu aliuawa kwa upanga huko Uhabeshi (Ethiopia ya leo) baada ya kuonyesha imani kali dhidi ya kanisa la Kristo. Alijeruhiwa kwa upanga na kidonda chake hakikupona hadi umauti ulipomfika.

2. #Marko
Huyu alifariki huko Alexandria Misri ya sasa baada ya kuangushwa na farasi barabarani, aliangushwa vibaya na hakupata msaada. Mwishowe akafariki.

3. #Luka
Alinyongwa huko Ugiriki, hii ni kutokana na msimamo wake mkali aliouonesha dhidi ya Kristo.

4. #Yohana
Huyu alitumbukizwa katika pipa lenye mafuta yanayochemka huko Roma, (Italia ya sasa). Hata hivyo kwa miujiza hakuungua na alitolewa akiwa mzima kabisa.

Alipelekwa katika gereza lililokuwa katika migodi huko kisiwa cha Patmos. Na huko ndiko alipofunuliwa na mwenyezi Mungu na kuandika kitabu cha "Ufunuo wa Yohana". Baadae aliachiwa huru na kwenda kutumika kama Askofu huko Edessa (Uturuki ya sasa). Alifariki akiwa mzee sana. Na ni mtume pekee aliuefariki bila mateso.

5. #Petro
Huyu alipata adhabu ya kifo cha msalaba. Ila yeye alisulubiwa tofauti na Yesu kristo. Kusulubiwa kwa Petro ilikuwa kichwa chini miguu juu katika msalaba wenye nembo ya "X". Petro mwenyewe aliomba asulubiwa kwa namna hii kwani hakutaka kusulubiwa kama Yesu (Yohana 21:18).

6.#Yakobo
Alikuwa Kiongozi wa kanisa huko Jerusalemu Israel ya sasa. Yeye alitupwa kutoka juu kabisa ya mnara wa hekalu wenye urefu wa meta 100 baada ya kugoma kumpinga Kristo. Mnara huo ni ule ambao Shetani aliutumia kumjaribu Yesu kwa kumwambia kama yeye ni mwana wa Mungu ajirushe. Walipogundua kuwa hajafa baada ya kumdondosha tokea juu ya mnara, walimpiga na mawe mpaka akafa.

7. #Yakobo (mwana wa Zebedayo)
Alikuwa ni mvuvi kabla Yesu hajamteua kuwa mwanafunzi wake. Akiwa kiongozi mkubwa wa kanisa Yakobo alichinjwa huko Jerusalemu kwa kukatwa kichwa kwa amri ya Herode (Matendo 12:2).

8. #Batholomayo
Pia alijulikana kama Nathanieli. Alikuwa ni mmisionari huko Armeni (Asia ya sasa). Alimshuhudia Yesu Kristo huko Uturuki. Yeye aliuawa kwa kupigwa fimbo baada ya kugoma kuacha mafundisho yake dhidi ya Kristo.

9. #Andrea
Aliuawa kama Petro huko Ugiriki kwa kusulubiwa kwenye msalaba wenye umbo la "X" miguu juu kichwa chini sawa na Petro Petro. Ila baada ya kuwambwa msalabani aliendelea kupaza sauti akihubiri neno la Mungu mpaka mauti ilipomchukua. Akiwa msalabani aliwaambia wafuasi wake "nilikua naisubiri saa kama hii"

10. #Tomaso
Aliuwa kwa kupigwa na mshale huko Chennai (India ya sasa) katika moja ya safari zake kama Mmisionari kwenda kuanzisha Kanisa huko.

11. #Yuda (Thadei)
Aliuawa kwa kupigwa na mshale ubavuni.

12. #Yuda (Iskariote)
Huyu alijiua kwa kujinyonga baada ya kumuuza Yesu kwa vipande 30 vya fedha.

NOTE:
13. #Thadayo (au Mathia) ni Mwanafunzi aliyeteuliwa na Yesu kuziba nafasi ya Yuda Iskariote (msaliti). Huyu alipigwa na mawe hadi kufa na baada ya hapo walimkata kichwa.

14. #Paulo
Hakuwa mmoja wa wale wanafunzi 12 wa Yesu. Lakini huhesabika kuwa mfuasi wa Kristo na mtetezi wa mwanzo wa Kanisa. Huyu aliteswa na baadaye akachinjwa na Emperor Nero huko Roma mwaka (A.D).

Kabla ya kuchinjwa Paulo aliishi muda mrefu sana gerezani ambapo akiwa huko aliandika barua (nyaraka) nyingi kwa makanisa mbalimbali. Ndio hizi ambazo zinafundisha misingi ya ukristo katika agano jipya, kama vile Waraka wa Paulo mtume kwa Warumi, Wakoritho, Waefeso, Wakolosai, Wathesalonike, Timotheo etc.

NB: Si muhimu kujua ni namna gani mitume walikufa, ila ni muhimu kujua kuwa mitume wote walikufa wakitetea imani yao. Walikua tayari kuchukiwa na kufa vifo vya mateso kwa ajili ya kumtetea na kumshuhudia Kristo.

Biblia imesema, "Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu, lakini mwenye kuvumilia mpaka mwisho, ndiye atakayeokoka." Mathayo Mtakatifu 10:22

Sent from my SM-A715F using JamiiForums mobile app
 
Hypocist focused on individual's targets shall spoil the African Nations no matter what.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…