Kifupi tu hakuna mtu au kampuni inaweza kudhibiti mizigo kila inakotoka kwa sababu ukakasi wa miliki ya miundombinu, sheria za kodi na mipaka ya nchi itamkwamisha.
Barabaraba au reli mbovu ataendesha pia ujenzi wa barabara na reli ikiwa na usimamizi wake.
Kama kuna kodi za kukusanya na anaona ni mwendo wa konokono atachukua majukumu ya TRA, TANROADS TRL n.k ili kuharikisha shughuli zake.
Kama sheria za miliki ardhi ni kikwazo cha bandari kavu au kuongeza maeneo ya kukuza shughuli zake itabidi hata bunge lijiuzulu na kumpisha mwekezaji aunde bunge lake na kugeuza sheria tajwa?
Kama hayo hayatoshi khoja za mapato zaidi zinalinganishwa na nini?
Mkataba feki hauna malengo ya kimapato sasa wenzetu hayo matrilioni mnayatoa wapi kwani mkataba upo kimya juu ya wajibu wao lakini bado tunaendelea kupotoshwa na hizi chambo feki.
HATUNASWI!
La nyongeza, kasi ya kupandishwa na kuongezwa kwa viwango na aina ya kodi ni ushuhuda tosha uwekezaji ndiyo umeshindwa siyo sisi tumeshindwa.
Hivi haya mashimo ya machimbo ya madini bado tunahitaji ushahidi upi kuthibitisha ya kuwa ahadi za matunda ya uwekezaji hayapo?
Ni lini hawa wanaoshabikia uwekezaji watarudi na kueleza mafanikio waliyotuahidi tangia enzi za Mkapa hadi leo na kwanini kodi bado tunalipa?
Malengo ya uwekezaji angalau yangelituondolea mzigo wa kodi lakini kinyume chake yameongeza kasi ya kutubebesha mizigo ya kodi.
Nchi hii kamwe haitaendelezwa na wawekezaji bali itaendelezwa na sisi watanzania wenyewe.
Historia ya uwekezaji Tanzania hawako tayari kulipa kodi huo ndiyo ukweli.
Hawa DP WORLD wako wazi hawatalipa kodi kwani mkataba unasema sheria za kuwalinda wawekezaji wasilipe kodi zitatumika na wala hawana kifungu hata kimoja kinachowashurutisha kuchangia bajeti ya nchi hii
La ajabu wanaotuingiza huu mkenge wanawatupia lawama wataalamu waliowateua wao wenyewe ya kuwa wamegeuza taasisi za umma kuwa shamba la bibi.
Swali ambalo wanalikwepa ni nani kawawezesha kuigeuza nchi kuwa shamba la bibi?
Majibu mnayo acheni shobo hizi.
Mnawapa maswahiba wale halafu wakiitafuna nchi mnawageuka wakati wametimiza malengo [emoji2] [emoji3] [emoji1] [emoji16]