Halafu baada ya nondo nzito hizi akatuvamia na mkataba wa kuitengua katiba ya JMT pale ambapo sehemu ya nchi haiwajibiki kwa katiba yetu na sheria zake sasa hilo eneo limerudishwa kwa mkoloni wa kiingereza.
Kutumia sheria za uingereza kwenye nchi huru kama hii ni makosa ya uzandiki, ufedhuli na uasi usio na kifani na wahusika wote kama wangelikuwa wanajiheshimu wangelikuwa wamebwaga manyanga lakini kama Mwenyezi Mungu hawamwogopi iwe utu wao?
Unaapa kuilinda na kuiheshimu katiba ya JMT halafu unasaini mkataba ambao hauwajibiki kwa katiba uliyoapa na sheria zitokanazo na hiyo katiba.
Katiba yetu inaelekeza nchi hii itaongozwa na katiba hiyo wewe unaafiki kuikiuka katiba kwa kuridhia katiba ya mkoloni isimamie njia kuu za uchumi wa nchi hii.
Haya yote wayatenda na huoni soooooo na kuachia ngazi.
Katiba yetu ndiyo mhimili wa mali zetu sasa sheria za mkoloni wapi na wapi?
Kama sheria za mkoloni ni bora kulinda utajiri wetu kuliko zetu kwanini tunajitawala?
Kwanini haturudi UN na kukiri Nyerere aliongopa HATUKO TAYARI KUJITAWALA?
Tuvunje bunge na serikali yote na Mwingereza akamate usukani.
Hatuwezi kuleta ubaguzi wa baadhi ya maeneo yanawajibika kwa sheria za nchi hii na baadhi ya maeneo hayawajibiki.
Katiba yetu inakataza ubaguzi wa aina zote na mikataba inayoitengua katiba yetu kutawala nchi hii kwa sheria zetu na maazimio ya kifisadi ya Bunge yanayobariki udhalilishaji wa aina hii mahakama lazima itengue nchi irudi njia kuu.
Huu mchepuko tunaukemea turudi njia kuu ya kuwaamini watanzania wanaweza kusimamia mambo yao yote