New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

Pamoja na Jaji wa mahakama ya Rufaa Mugasha kuhoji kuongezewa muda Jaji Mkuu kwa kuongozwa na barua ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa wakati ule lakini katiba inamruhusu Rais kumwongezea muda wa utumishi Jaji yeyote yule kama anaona ni kwa masilahi ya taifa kwa kufanya hivyo. Sasa kujikita kwenye barua ya AG wakati katiba ipo sijui maana yake ni nini
 
Makusanyo ya kodi ikiwemo TRA ni swala la Muungano hivyo uteuzi huu umezingatia sheria.


Tatizo wao kwenye katiba yao wanajiita ni nchi sasa huku wanasaka tonge la pili.

Baada ya Zanzibar kujiita ni nchi ilipaswa katiba irekebishwe na muundo uwe wa shirikisho maana mshirika mmoja kajitoa kwenye Muungano




 
Bandari ni suala la Muungano lakini serikali ya Zanzibar inajitegemea na imeingia mkataba na Qatar kwa miaka 5. Sasa kama Zanzibar hawako chini ya TPA basi katiba hii imekiukwa na inaleta maswali mapya uhalali wa Wazanzibara kuongoza wizara ya uchukuzi wakati kiutendaji siyo suala la Muungano
 
Katiba ya Zanzibar imeukana Muungano lakini wadanganyika tunaendelea kujidanganya tupo kwenye Muungano wakati hatuko huko.

Katiba ya Zanzibara imetamka wao ni nchi sasa kama wao ni nchi ina maana hatuna Muungano bali tumo kwenye serikali ya shirikisho la nchi mbili.

Muungano maana yake nchi zilimezwa na muungano wakati ndivyo katiba ya JMT inavyoongea lakini kiutelekelezaji Zanzibar hawautaki Muungano ila tu unapowapa ulaji tu.

Sasa kwa vile, wao hawatutaki ni vyema tukaona umuhimu wa kupiga kura ya kama kwanza pande mbili za Muungano wanauhitaji na kama hawauhitaji uvunjwe na kama sote tunauhitaji basi tukubaliane liwe shirikisho la nchi mbili badala ya kujiita Muungano wakati haupo.



Wazanzibara wako kwenye Muungano kuula tu kwa hiyo siyo wazalendo na ndiyo maana wanatuuza kama njugu.
 
"Mtanzania ninamfananisha na bwege mmoja ambaye aliokota almasi kubwa lakini chafu chafu. Mjanja mmoja (mwekezaji) alipoona hivyo naye akaokota kichupa akakichonga ma kukisafisha na akamfuata bwege na kumshawishi wabadilishane. Bwege alipoona kichupa mbona kinang'aa akakubali akapewa kichupa tu ili mradi kinang'aa na mwekezaji akaishia na almasi akaenda kuiosha na kuichonga na ikang'aa zaidi ya kile kichupa...bwege alipoona almasi yake imeng'aa akakitupa kile kichupa kikavunjika vunjika na yule mjanja akamwambia ukitaka almasi yako itabidi unifidie kwa uwekezaji wangu na gharama ya fidia ni kukuuzia hii almasi kwa bei ya soko.....bwege alipigwa na butwaa....hakuamini alivyotapeliwa." - J.K. NYERERE

Mfano hai.


Mtanzania (bwege) alimwuuzia Kaburu NBC kwa bei ya kutupwa ya dola milioni 300 baadaye bwege akagundua alimwuuzia benki mbili kwa bei ya benki moja. Bwege huyu Mtanzania alipotaka arudishiwe benki ya NMB kaburu (mjanja) akamwambia amerudishie zile dola milioni 300 alizonunulia benki zote mbili ili amwuuzie NMB.

Bwege (Mtanzania) akakubali na hivyo akauzia benki yake mwenyewe kwa hela aliyouzia benki mbili na hivyo kaburu akawa kajinyakulia NBC bure bila ya hata ya kulipa hata senti moja.

Kama hilo halitoshi baada ya miaka nenda rudi kaburu akamwuuzia mwingereza NBC kwa bei ambayo hadi leo haijulikani na kuinyima TRA mapato ya kodi.


Kama hili halitoshi, bwege sasa kauza bandari kwa bei ya kutupwa yaani hata sumni hatalipwa na kuna siku atashtuka kaingizwa mkenge na kwa sababu wako waliohongwa wakachukua hela sasa mwekezaji mwarabu atadai fidia ya mabilioni ya dola sawasawa na bei ya sokoni ya bandari zetu na wengi leo wanapigia upatu wizi wa mali ya umma watakuwa aidha hawako madarakani au watakuwa wametulizwa kwenye makaburi yao na kuwaachia vizazi vijavyo mgogoro mkubwa wa kimkataba
 
Major projection: SISIEMU WAKO DUBAI KUWAPIGIA MAGOTI WAARABU VIFUNGU VIFUATAVYO VYA MKATABA WA KIMATAIFA IGA VIREKEBISHWE!




Katika khali ya sintofahamu ya kisiasa na vuguvugu lake ambalo sasa limegeuka mtaji wa kisiasa wa wapinzani kuing'oa sisiemu madarakani na wao wamejibu mapigo kama ifuatavyo:-


A) Wamerudi Dubai na kumwomba Mtawala wa hilo jimbo hilo aridhie marekebisho ya mkataba yafuatayo:'-

Moja, Hii IGA isainiwe na Falme za Kiarabu na kutengua khoja Dubai siyo nchi,

Mbili, IGA au mkataba uwe na ukomo wa miaka 20 - 25 ili kuondoa khoja bandari zetu zote zimeuzwa,

Tatu, kutamka waziwazi kwenye hiyo IGA bandari zimekodishwa, haziuzwi wala kubinafsishwa,

Nne, Kuweka wazi mkataba huu utahusu bandari ya Dar-es-Salaam tu bila kuhusisha bandari nyingine zozote zile


Tano, airspace au anga na mapito ya mizigo pia kunyofolewa kwenye mkataba kama wataridhia marekebisho hayo,

Sita, kuonyesha kiasi maalumu kwa mwaka Tanzania itapata kisipungue mapato ambayo sasa hivi inapata na kuonyesha ndani ya miaka 10 mapato kwa mwaka kuongezeka mara mbili au zaidi ya haya yaliyopo,

Saba, TRA kuendelea kukusanya kodi kama sheria za kodi zinavyoagiza,

Nane, vyombo vya usalama kuendelea na shughuli zao kwenye bandari husika,

Tisa, kuondoa vipengele vinavyoitaka serikali yetu kuijuza serikali yao juu ya fursa za uwekezaji nchini,

Kumi, kuiondoa kampuni ya DP World kwenye mkataba wa kimataifa wa IGA kwa minajili ya kutengua khoja ya sheria zetu hususani zinazokataza upendeleo na kuzima ushindani zilikiukwa kwa kuwapa DP WORLD upendeleo tajwa.


Kama vipengele hivi 10 Mtawala wa Dubai ataafiki na kurekebisha mkataba huu wa kimataifa inamaanisha ile kesi ya akina msomi Mwabukusu itaachwa kwenye mataa kwa maana itakuwa imepitwa na wakati.


Nionavyo Mtawala wa Dubai ataafiki si unajua ile riwaya ya mwarabu na ngamia kwenye hema?

Ngamia alimwomba mwarabu aingize kichwa tu mwishowe alimtimua mwarabu kwenye hema.

Dubai mkakati wao waingize pua tu baadaye nchi yote wataichukua
 
Mwiba: A Tanzanian wildlife ranch under lease to American billionaire’s company.

Dar es Salaam. Tanzania is home to one of the best wildlife reserves in Africa, making it a revered safari destination for many across the world, but not much is known about Mwiba Wildlife Ranch, a property leased to Mwiba Holdings Limited, owned by American billionaire Dan Friedkin.

The Texas-based businessman, who is also the chairman of Gulf States Toyota, is the beneficial owner of Mwiba Holdings Ltd.

According to their local representatives, the area was acquired in 2008 on a 30-year lease after an agreement was reached between Makao Village Council and Meatu District Council.


"Mwiba Holdings Ltd operates the ranch and has been paying annual land rental and servicing the lease agreement for the 48,548 acres for the Mwiba Ranch, 10,872 acres for Mwangundo, and 112,183 acres for the Makao WMA," says the representative.

Spread over thousands of acres, Mwiba borders the Ngorongoro Conservation Area’s western boundary and the southern part of Serengeti National Park.

Serengeti’s wildebeest migration passes through Mwiba between December and April. Characterized by rolling hills, kopjes, thickets, waterholes, and (dry) rivers where pools form, its permanent water attracts wildlife all year round.

Visitors who have been there say it is an animal magnet when the southern Serengeti and the Ngorongoro Conservation Areas dry out between July and November each year.

The Mwiba Lodge, an eye-catching beauty that complements the area, costs $1,800 per person and was built with a near-stealth presence in the landscape.

Though an article in Forbes says the billionaire’s family trust, the Friedkin Conservation Fund (friedkinfund.org), has leased an astonishing 6 million acres of Tanzania's wilderness with an eye towards protecting it, his representatives have refuted the claims.

"Friedkin Conservation Fund is a charity organization whose trustees are Tanzanians, with Dan Friedkin as the sponsor of the trust to support wildlife conservation and community development," he says.

He named the trustees as Abdulkadir Luta Mohammed, Asela Msando, and Naib Sykes and further clarified that Mwiba Holdings is a wildlife ranch that belongs to Makao Village Council as the owner.
 
Big projection


Tulia Ackson kuwa spika wa kwanza kupoteza jimbo la uchaguzi 2025!



Nimetafakari mambo mawili moja nini kilitokea uchaguzi uliopita na khali ya kisiasa ya sasa namwona Mhe. Tulia Ackson kudondoshwa ubunge na Msomi Boniface Mwabukusu.


Namwona Spika kuendelea kuwa spika hata baada ya kuanguka ubunge wa jimbo la uchaguzi wa Mbeya mjini kwa sababu ya mchango wake wa kupitisha Azimio la bunge la mkataba wa kuuza bandari zetu.

Hahitaji pia kiwa mbunge kuwa spika ingawaje baada ya kuanguka atakuwa kadhoofika kisiasa.


Na pia nawaona sisiemu kumfyagilia Msomi Mwabukusu kwa kumfutia leseni yake ya uwakili na kumtajataja kila mahali.

Bila kujijua wanampigia bonge la kampeni ya kuwa mbunge.

Yule mwanamuziki wa kufokafoka najua anakinyemelea kiti lakini wapigakura wanataka damu mpya kwenye siasa za jimbo lao.

Hivyo, Sugu hatakuwa mbunge ataanguka kwenye kura za maoni za CDM labda Tulia afanikiwe kuongeza majimbo basi naye Sugu atapata la kwake.


Ninawakilisha.
 
UFISADI WA KUTISHA EWURA SIYO KUPAA KWA DOLA CHIMBUKO LA KUPANDA BEI YA MAFUTA


EWURA wamewakumbatia BULK SUPPLIERS wako takribani 5 na wengi wao wana asili ya India. Hawa wazabuni hukaa na kupanga bei ya kuuza mafuta kwa bei waitakayo na hivyo kutufukarisha lakini baadhi ya wenzetu walioko EWURA na Wizara ya Nishati wamevuna utajiri wa kutisha.


Maswali 9 yafuatayo EWURA kamwe hawawezi kuyajibu nayo ni:-

Kwanza, EWURA watupe sababu za mafuta kuagizwa kutoka India ambao ni wachuuzi tu wa mafuta kutoka Urusi?

Pili, kwanini EWURA hawanunui mafuta moja kwa moja kutoka Urusi ambapo pipa moja la lita 100 lauzwa dola 30 chini ya bei ya soko la dunia?

Tatu, kwanini EWURA ni walaini sanaaaaaaa kuitia hasara taifa kwa kununua mafuta bei ambayo ni juu ya bei ya soko? India inaponunua mafuta ya Urusi kwa punguzo la dola 30 hilo punguzo hawalipeleki kwa walaji bali hubaki nalo. Pia, wanaweka kodi zao sasa ukichanganya na ufisadi uliomo humo na kodi zetu bei ya mafuta kwa mlaji lazima iwe ya juu kupindukia!

Nne, kwanini wazabuni wanaoshinda zabuni hujirudiarudia makampuni yaleyale kama hayajajijengea mtandao hapo EWURA na Wizara husika?

Tano, kwanini EWURA wao wenyewe wasiagize mafuta kutoka Urusi na kupata punguzo la dola 30 kila pipa na kuachana na kodi za India na ufisadi wao?


Sita, kwanini serikali bado imeweka kodi za EWURA katika ankara za umeme wakati wanao uwezo wa kujiendesha yenyewe? Tunasema ruzuku kwa EWURA kumechangia sana kuuwa ubunifu maana wanashawishika kuweka mbele ufisadi wao na masilahi ya taifa baadaye wakijua tutawazawadia kwa kufanya hivyo kupitia ruzuku za kodi mbalimbali.

Saba, hivi ni wahindi tu ndiyo wenye uwezo wa kuagiza mafuta?

Nane, kwanini tununue mafuta kwa dola wakati Urusi wako tayari tununue mafuta kwa hela zetu za madafu? Hivi kwanini bado tunaongelea dola wakati tupo dunia ya BRICS?

Kwanini tunakiuka sheria ya kodi kwa kupachika kodi za EWURA, REA na pango juu VAT 18% ya bei za umeme na kuongeza mzigo kwa wazalishaji hasa wa umeme. Kwanini VAT 18% isikatwe kupata mapato ya EWURA, REA na kodi za mapango?

Ninawakilisha
 
 
Mgombea Urais alikiri hajui alipata kura ngapi uchaguzi uliopita kwa utetezi ya kuwa hata Tume ya uchaguzi haijabamdika matokeo ya kila jimbo kwenye tovuti yao kama sheria za uchaguzi zinavyosema.

Tunasema hii inashangaza tukizingatia baada ya uchaguzi alikuwa mstari wa mbele kutuhimiza tuandamane kupinga matokeo ya uchaguzi wa 2020 wakati yeye mwenyewe hakuwa na takwimu zozote za kumfanya akhoji uhalali wa matangazo yaliyotangazwa.

Alipaswa yeye na chama chake wawe na utaratibu wa kukusanya matokeo na fomu zake kila kituo na kufanya majumuisho yake ili kuwa na takwimu za kuwaongoza kwenye maamuzi yao.
 
Tweet by Onesmo Mushi @EduTalkTz

UMEKAA KIMYA KAMA HAYAPO

1. Mafuta yanapandishwa Bei kiholela kutoka 2700 mpaka 3100, UMENYAMAZA.

2. Bandari zetu zinapeanwa kwa Waarabu kwa mkataba wenye vipengele vya HOVYO kabisa, UMENYAMAZA.

3. CAG anatangaza mabilioni ya fedha za watanzania maskini zinafujwa na kuibiwa na watawala wachache kila kukicha, UMENYAMAZA.

4. Wamasai kule Ngorongoro wanaporwa ardhi yao, wananyang’anywa mali zao, na kunyanyaswa kama wakimbizi kwenye nchi yao, UMENYAMAZA.

5. Wabunge wanajiongezea posho na mishahara kutoka milioni 12 mpaka milioni 16 kwa mwezi na kujilipa 470,000 kila siku ya Mungu huku watoto wetu wakishindwa kujengewa hata matundu ya vyoo mashuleni, UMENYAMAZA.

6. Viongozi wanaonesha dharau ya wazi kwa umma na kujibu arrogantly pale wanapoulizwa maswali ya msingi na umma na kutoa kauli Kama vile “HAMIA BURUNDI,” UMENYAMAZA.

7. Vyombo vya habari vilivyopewa imani ya umma Kwa mategemeo kwamba vitapigania maslahi ya umma vinageuka kuwa vuvuzela za watawala, UMENYAMAZA.

8. Rais anagawa fedha za umma kwa timu za Simba na Yanga kwa maslahi yake ya kisiasa huku watoto wetu mpaka leo wakikosa vitabu na madawati, UMENYAMAZA.

9. Rais anatumia mabilioni ya walipa kodi kugharamia vitu vya HOVYO kama filamu ya Royal Tour na nyingine akila bata na jopo lake kama alivyofanya NewYork wakati watanzania wanakufa kwa kukosa vifaa tiba, UMENYAMAZA.

10. Viongozi wanatumia zaidi ya Bilioni 500 kwa mwaka kununua magari ya kifahari na kuishi maisha ya anasa kwa kodi na tozo unazolipa wewe unayeishi maisha ya dhiki kubwa, UMENYAMAZA.

11. Serikali inatumia jeshi la polisi @tanpol , mahakama, na vikundi vya kigaidi kuwadhuru wale wanaopigania maslahi yako ili kuwanyamazisha na kuendelea kukunyonya, UMENYAMAZA.

12. Serikali inageuza huduma za afya kuwa biashara inayowaneemesha wachache na kuyaweka maisha yako rehani, BADO UMENYAMAZA.

13. Watoto wako wanalazimishwa kufanya kazi hatari kabisa kwenye maisha yao kama bodaboda na wengine wengi wakisukumiwa kwenye biashara hatari kama biashara za ngono, madawa ya kulevya, ujambazi etc., huku watoto wa viongozi wakiandaliwa kushika dola, wewe UMENYAMAZA.

14. Kiongozi anayejipambanua kwamba anawakilisha malalamiko yenu kwa serikali anafanya kazi ya kulala tu bungeni @bunge_tz na kupiga makofi bure, wewe UMENYAMAZA.

15. Kama haitoshi, serikali inaminya uhuru wako wa kujieleza na kutoa maoni, inakulazimisha kuvumilia maumivu na kukupangia namna ya kulia pale unapotaka kupiga kelele za malalamiko kwa hoja kwamba “UNATAKIWA KULIA KWA STAHA” wewe UMENYAMAZA.

WEWE NANI SASA
1. My friend, ashakum si matusi, WEWE NI KIKWAZO CHA MAENDELEO YA TAIFA LA TANZANIA. 2. NA KAMA NI “MSOMI” na unaNYAMAZIA yote haya, WEWE NI MZIGO KWENYE HII NCHI.
 
Tweet by Onesmo Mushi @EduTalkTz

UMEKAA KIMYA KAMA HAYAPO

1. Mafuta yanapandishwa Bei kiholela kutoka 2700 mpaka 3100, UMENYAMAZA.

2. Bandari zetu zinapeanwa kwa Waarabu kwa mkataba wenye vipengele vya HOVYO kabisa, UMENYAMAZA.

3. CAG anatangaza mabilioni ya fedha za watanzania maskini zinafujwa na kuibiwa na watawala wachache kila kukicha, UMENYAMAZA.

4. Wamasai kule Ngorongoro wanaporwa ardhi yao, wananyang’anywa mali zao, na kunyanyaswa kama wakimbizi kwenye nchi yao, UMENYAMAZA.

5. Wabunge wanajiongezea posho na mishahara kutoka milioni 12 mpaka milioni 16 kwa mwezi na kujilipa 470,000 kila siku ya Mungu huku watoto wetu wakishindwa kujengewa hata matundu ya vyoo mashuleni, UMENYAMAZA.

6. Viongozi wanaonesha dharau ya wazi kwa umma na kujibu arrogantly pale wanapoulizwa maswali ya msingi na umma na kutoa kauli Kama vile “HAMIA BURUNDI,” UMENYAMAZA.

7. Vyombo vya habari vilivyopewa imani ya umma Kwa mategemeo kwamba vitapigania maslahi ya umma vinageuka kuwa vuvuzela za watawala, UMENYAMAZA.

8. Rais anagawa fedha za umma kwa timu za Simba na Yanga kwa maslahi yake ya kisiasa huku watoto wetu mpaka leo wakikosa vitabu na madawati, UMENYAMAZA.

9. Rais anatumia mabilioni ya walipa kodi kugharamia vitu vya HOVYO kama filamu ya Royal Tour na nyingine akila bata na jopo lake kama alivyofanya NewYork wakati watanzania wanakufa kwa kukosa vifaa tiba, UMENYAMAZA.

10. Viongozi wanatumia zaidi ya Bilioni 500 kwa mwaka kununua magari ya kifahari na kuishi maisha ya anasa kwa kodi na tozo unazolipa wewe unayeishi maisha ya dhiki kubwa, UMENYAMAZA.

11. Serikali inatumia jeshi la polisi @tanpol , mahakama, na vikundi vya kigaidi kuwadhuru wale wanaopigania maslahi yako ili kuwanyamazisha na kuendelea kukunyonya, UMENYAMAZA.

12. Serikali inageuza huduma za afya kuwa biashara inayowaneemesha wachache na kuyaweka maisha yako rehani, BADO UMENYAMAZA.

13. Watoto wako wanalazimishwa kufanya kazi hatari kabisa kwenye maisha yao kama bodaboda na wengine wengi wakisukumiwa kwenye biashara hatari kama biashara za ngono, madawa ya kulevya, ujambazi etc., huku watoto wa viongozi wakiandaliwa kushika dola, wewe UMENYAMAZA.

14. Kiongozi anayejipambanua kwamba anawakilisha malalamiko yenu kwa serikali anafanya kazi ya kulala tu bungeni @bunge_tz na kupiga makofi bure, wewe UMENYAMAZA.

15. Kama haitoshi, serikali inaminya uhuru wako wa kujieleza na kutoa maoni, inakulazimisha kuvumilia maumivu na kukupangia namna ya kulia pale unapotaka kupiga kelele za malalamiko kwa hoja kwamba “UNATAKIWA KULIA KWA STAHA” wewe UMENYAMAZA.

WEWE NANI SASA
1. My friend, ashakum si matusi, WEWE NI KIKWAZO CHA MAENDELEO YA TAIFA LA TANZANIA. 2. NA KAMA NI “MSOMI” na unaNYAMAZIA yote haya, WEWE NI MZIGO KWENYE HII NCHI.
 
Asilimia 90 ya wabunge wa CCM kupoteza ubunge wao chaguzi za 2025!


Pamoja na wabunge wa CCM kuuza bandari zetu zote bwerere na kutukejeli sisi ni vilaza tunaohitaji darasa kutoka kwao huku wakijipandishia mishahara na posho kimya kimya wakati ya wengine hawajali lakini wana khali mbaya ya kisiasa majimboni kwao.


Wengi wao wanadiriki kusema wanachukua kiinua mgongo chao ikiashiria wanajua hata kwenye mchakato wa kua za maoni ndani ya CCM hawatabaki salama.


Katika khali hii ya kutojiamini na kukata tamaa ni dhahiri ni vigumu kwa waheshimiwa hawa kupigania masilahi ya taifa na ndiyo maana wameweka mbele matumbo yao.


Wabunge karibu wote wa CCM baada ya kubaini hawauziki wala kuchagulika majimboni mwao ndiyo maana wanakubali kila kitu ili wabebwe na kamati kuu ya CCM pale watakapogalagazwa kura za maoni


Kila mbunge kawa chawa wa mama badala ya kuweka masilahi ya wapigakura wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…