Ukisoma uzi wa ufugaji kuku aliotoa Mzalendo unaweza kucheka, kwa sababu alisema ukweli kwamba alianza na kuku mmoja tena jogoo,baadae alimla. Hii style ni nzuri kwa sababu, kwanza inakuondoa kwenye nadharia na kukupeleka kwenye vitendo. Imebidi nii-copy na kui-paste kwangu. Nimenunua ng`ombe mmoja tu chotara aliyepandishwa. Kwa wale wanaopenda kufuga ng`ombe basi tuwasiliane hapa hapa jamvini. Mzee aliyeniuzia mimi ana ng`ombe wengi wazuri na bei yake ni nzuri.