Nadhani tuiachie Mahakama kutekeleza wajibu wake.
I guess na Kikwete tumuachie kuongoza nchi, tusi comment chochote kile, au?
By the way, hii affidavit inasema
"As a consequence...The accused were thus arrested and charged with the offences contained in the charge sheet." Tungepata hiyo charge sheet tungeelewa zaidi ni specific offences gani, vipengele vya sheria gani vimevunjwa. Tujue hiyo sheria ya "kusababisha hasara" wametumia ipi hiyo.
Tunaambiwa makosa ya "kusababisha hasara," hawa wadau, especially Yona (na mipango yake na Mkapa), hawakufanya uzembe uzembe kwa bahati mbaya na kusababisha hasara; walinuia kujinufaisha kwa kupanga. Tuseme ni wezi, sio wazembe. Vinginevyo waachiwe huru mapema, tusifanyiwe usanii.
Sheria aliyoharibu Mramba, kwa mfano, ya misamaha ya kodi, inasema wazi kwamba maofisa wakifanya madudu pasipo nia mbaya hawana hatia, vipengele 4, 12, Invesment Act, 1997:
A member, officer or other staff of the Tanzania Investment Centre shall not in his personal capacity be liable in civil or criminal proceedings, in respect of any act or omission done in good faith in the exercise of his functions under this Act ...The Centre shall be an Agency of the Government and shall be under the general supervision of the Minister.
Sasa hapo Mramba kama msimamizi mkuu wa hii investment center anaweza kujaribu kujitetea kuwa na yeye analindwa na hii "good faith" exception. Kwamba alisamehe kodi sio kujinufaisha bali kuvutia wawekezaji.
Kama wamejinufaisha tuseme wamekwiba, sio wazembe.